Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?
SURATUL-IKHLAS.
Inaelezwa kuwa walimfuata Mayahudu kumfata mtume (s.a.w) na kumwambia awasifie namna ambavyo Mola wake alivyo ndipo Allah akaishusha sura hii. Pia katika kauli nyingine ni kuwa Makafiri waliokuwa wakiabudia masanamu walimwendea Mtume (s.a.w) na kumwambia awaeleze sifa na namana Mola wake alivyo ndipo Allah akateremsha sura hii. Sura hii ni katika sura za mwanzo kabisa kushuka Makka na mafundisho yake yanavunja kabisa ibada ya masanamu na Ukristo na kila mafundisho ya miungu wengi.
Mama Aisha anasimulia ya kwamba Mtume s.a.w. alipokuwa akienda kitandani kwake kila usiku, aliunganisha vitanga vya mikono yake, kisha anavisomea Qul huwallaahu na Qul a'uudhu birabbil falaq na Qul a'uudhu birabbinnaas, na anavipulizia, kisha anavipaka mwili wake wote kila anapoweza kupagusa toka kichwani; na akifanya hivyo mara tatu (Bukhari jalada la 3).
FADHILA ZA SURAT AL-IKHLAS
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Sura hii inazungumzia kuhusu hali ya Abulahab namke wake wakiwa kama Watu waovu. Ni moja katika sura ambazo zilishuka mwanzoni toka Mtume alipoamrishwa kulingana dini kwa uwazi.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Aina za idgham ni idgham al mutamathilain, na idgham al mutajanisain
Soma Zaidi...3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran??
Soma Zaidi...