Menu



Sababu za kushukasurat an Nasr

Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W

Sababu za kushuka surat an-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR
Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.a.w) hupo maka wakati wa hija ya mwisho, hija ya kuaga. Sura hii matika mashafu imewekwa katika sura za Madina kwa sababu imeshuka wakati mtume ameshafanya hijira kwenda madina.


 

Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Sura hii imekuja kutabiri kifo cha Mtume (s.a.w).


 

Kutokana na mapokezi ya hadithi sura hii ndiyo sura ya mwisho kushuka katika quran ila sio aya ya mwisho kushuka. Sura hii ilishuka kwenye masiku ya tashriq katika mwezi wa dhul-hija. Baada ya kushuka sura hii Mtume (s.a.w) ndipo akahutubia waumini.

 

Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.


 

Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.

 

Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu


 

Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views 1669

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

quran na sayansi

YALIYOMONENO LA AWALI1.

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MADD YAANI KUVUTA HERUFI KWENYE USOMAJI WA QURAN

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka Surat al fatiha (Alhamdu)

Kwa kuwa hakuna sababu mwalumu ikiyonukuliwa kuwa ndio chanzo cha kushushwa suravhii. Basi post hii itakujuza mambo ambayo huwenda hukuyajuwa kuhusu fadhika za surabhii na mengineyo.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al-Fiyl

Al fiyl ni neno la Kiarabu lenye maana ya tembo. Sura hii inazungumziakisa cha jeshi lenye tembo. Jeshi hili lilikuwa na nia ya kuvunja al qaaba

Soma Zaidi...
Kwa nini quran ilishuka kidogo kidogo?

Kuna sababu nyingi za kuonyesha umuhimu wa Quran kushuka kwa mfumo wa kidogo kidogo

Soma Zaidi...
Aina za Madda twabiy kwenye usomaji wa Quran

Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy

Soma Zaidi...
Sababu za kushushwa kwa surat al-kafirum

SURATUL-KAFIRUN Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.

Soma Zaidi...
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...