Sababu za kupasuka kwa mfuko wa kizazi

Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.

Sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba mfuko wa kizazi yanani uterusi upasuka pale mama anapokuwa na uchungu, unaweza kupasuka mzima au akapasuka sehemu kidogo na mama akipata huduma ya haraka anaweza kutoa mtoto wake akiwa hai kabisa.

 

2. Sababu ya kwanza ni kuwepo kwa alama au kovu kwenye tumbo, kwa mfano labda mama kwenye mimba ya kwanza alifanyiwa upasuaji na akipatwa na uchungu akiwa mbali na hospitali na akakosa huduma ya haraka anaweza kupasuka mfuko wa kizazi.

 

3. Mtoto kushindwa kutoka kwenye via vya uzazi kwa kitaalamu huitwa obstructed labour kwa sababu pengine njia ni ndogo kwa hiyo mtoto ukaa humo na anajaribu kutoka lakini anashindwa na mda unaendeleaje bila msaada wowote hatimaye mfuko wa kizazi unapasuka.

 

4. Kusinyaa sana kwa mfuko wa kizazi.

Ili mama aweze kujifungua anapaswa kuwa na uchungu na uchungu huo utokea kwa sababu ya kusinyaa kwa mfuko wa uzazi, kuna kipindi uchungu inakosa na mama anapewa dawa aina ya oxytocin  ambayo Usababisha kusinyaa kwa mfuko wa uzazi na  ukisinyaa sana bila mpangilio usababisha kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

 

,5. Kwa hiyo baada ya kuona sababu hizo tunapaswa kuzitambua na kuzielewa vizuri na kuokoa maisha ya Mama na mtoto ili kuweza kumfanya mama ajifungue kwa urahisi zaidi.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/05/Sunday - 10:32:58 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1957


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-