Hii ni orodha ya dawa ambazo hutumiwa sana na watu kutoka maduka ya dawa lakini sio salama kwa wajawazito.
Post hii nineinukuu kutoka kwenye mtandao wa jamii forums. Kuna mdau alikuwa akielezea, nimependa maudhui yake na nikaona niilete ha hapa. Kama utahitajibkuisoma kw aurefu na kuangalia comment za wadau Bofya link hii https://www.jamiiforums.com/threads/dawa-kumi-ambazo-mama-mjamzito-hatakiwi-kutumia.1278149/
Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda
sana kuzitumia lakini bahati mbaya baadhi ya
dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito
kabisa kulingana na madhara makubwa
yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto
aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.
1.Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa
mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani
una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.
2.Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano (most common), mara nyingi hutumika
kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii
huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu
kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi
kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza
kusababisha mototo kuzaliwa akiwa hasikii yaani
kiziwi.
3.Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana
kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara
nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa
ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa.
Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na
huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.
4.Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa
mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama
capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika
kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya
huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa
mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na
kusababisha kuzaliwa na motto mwenye viungo
pungufu au zaidi.
5.Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni
salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi
mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza
kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya
mtoto[organogenesis} na kutoa motto asiye na
viungo vya kawaida.
6.Metronidazole au fragyl; hii dawa ipo kwenye
kundi la anti protozoa lakin pia hushambulia
bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua
minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko
wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi
mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa
utengenezaji wa viungo vya mtoto.
7.Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye
kikundi maarufu cha prostanglandins analogue,
hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi
kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu
madonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii
kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno
ikiwemo kutoa mimba kabisa.
8.Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo
humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi
tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha
kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata
matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio
dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.
9.Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu
minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za
maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama
wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa
mtoto.
10.Frusemide: hii ni dawa ambayo inapatikana
kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi
hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya
mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu
presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa
akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na
presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha
chini kabisa[intravascular volume depletion].
Together we can maintain healthy for the people
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii hasa inahusu kasoro ,utatuzi,na jinsi ya kutunga mimba kwa upande wa mwanamke na mwanaumeΒ .itatupelekea jinsi ya kuangalia kasoro na jinsi ya kutatua hizo kasoro katika jamii zetu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo mtu anapaswa kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili kisiweze kutokea na pia kama jamii ikishirikiana kwa pamoja tunaweza kuepusha kwa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Je na wewe ni moja kati ya wake ambao wanahitajivkujuwa siku za kupata mimba. Ama siku za competes mwanamke mimba. Post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Kipimo cha mimba kwa mkojo kimekuwa kikitumika sana kuangalia ujauzito. Kipimo hiki kinapotumika vibaya kinaweza kukupa majibu ya uongo. Kuwa makini na ujue muda sahihi.
Soma Zaidi...Mwanaume na mwanamke wanapo kutana na kujamiina kama mwanamke yupo kwenye ferlile process ni rahisi kupata mbimba. Sparm Zaid ya million moja huingia kwenye mfuko wa lakin sparm moja ndio huweza kuingia kwenye ovum(yai)lakin nyingine hubaki kwenye follopi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutoka kwa mimba, kwa kawaida tunafahamu kwamba mimba ikitungwa na mwili mzima huwa na wajibu wa kutunza kilichotungwa kwa hiyo ikitokea mimba ikatoka usababisha madhara yafuatayo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi.
Soma Zaidi...Mdau anauliza ni muda gani mwanamke anaweza kujijuwa kuwa amepata ujauzito.
Soma Zaidi...