Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?
Mimba ya namna hii kitaalamu hufahamika kama ectopic pregnancy. Je hii ni mimba gani? Hii ni mimba ambayo yai lililorutubishwa linaendelea kukuwa nje ya mji wa mimba (uterus). mimba inaweza kukuwa sehemu yeyote kwenye tumbo ila nje ya mji wa mimba. Kwa asilimia kama 90% mimba hukuwa kwenye mirija ya falopia. Hii ni mimba hatari sana na inahitaji uangalizi wa haraka sana, kwani inaweza kuhatarisha maisha ya mama. Inakadiriwa kuwa mimba za namna hii huchukuwa kati ya asilimia 1 mpaka 2 ya miba zote.
Kwa nini mimba hii ni hatari?
1.Mimba inatkuwa nje ya mji wa mimba hivyo haiwezekani mtoto kupona
2.Inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ama sehemu ilipokuwa.
3.Inaweza kusababisha ulemavu kwa mama endapo itachelewa kuonekana
4.Kwa asilimia 30 mimba hii haina dalili hii ni hatari zaidi.
5.Inaweza kusababisha uvujaji wa damu kwa kiasi ikubwa
6.Inaweza kusababisha mwanamke kuhitajiwa kufanyiwa upasuaji kamma tiba.
Sababu za kutokea mimba hii
Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa asilimia 30 ya mimba hizi hazina dalili. Lakini kwa kiasi kikubwa mimba hizi huwa na dalili. Tafiti zinaonyesha kuwa dalili zake hutokea kabla ya wiki ya 10. Sasa hapa nitakutajia baadhi tu ya dalili za mimba hii:-
1.Maumivu ya tumbo upande mmoja wa nyonga.
2.Maumivu ya mabega
3.Kutokwa na damu kwenye uke.
4.Maumivu ya nyonga.
5.Mvurugiko wa tumbo na kutapika
6.Maumivu ya upande mmoja wa mwili.
7.Kizunguzungu na uchovu
8.Maumivu ya mabega, shingo na mkundu.
Sababu za kutokea kwa mimba hii.
1.Kuwa na maambukizi kwenye via vya uzazi yaani PID
2.Uvutaji wa sigara
3.Kama una umri wa miaka 35 na kuendelea
4.Kama unatumia madawa ya kuivisha mayai
5.Kama ulishapata ujauzito huu hapo mwanzo upo uwezekano kuja kupata tena
6.Kama ulifanyiwa upasuaji kwenye mirija ya falopia
7.Kama una tatizo la endometriosis
8.Baadhi ya njia za kuthibiti uzazi mfano, IUD
Nini tena yapasa kujuwa?
1.Ujauzito uliotungia njea haurithiwi yaani kama mama aliwahikupata ujauzito huu hali hii hairithiwi.
2.Kutoka kwa ujauzito sio sababu ya kupata mimba hii
3.Kutoa ujauzito pia hakuna mahusianao na ujauzito huu
4.Mazoezi na michezo pia hihusiani na kutokea kwa ujauzito huu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu siku za kupata mimba na dalili za siku hizo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni.
Soma Zaidi...Mtoto huweza kuzaliwa ndani ya miezi 6 na unaweza kupona. Na huyu mdoe mtoto njiti. Na anaweza kuzliwa kwa njia ya kawaida. Hakuna ushahidi unaiinyesha kuwa njiti hukabiliwanamatatizo ya kitalima kwenye ukubwa wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi.
Soma Zaidi...Je unaijuwa siku yako hatari ya kupata mimba. Na itakuwaje kama tayari umebeba mimba changa. Nakala hii inakwenda kukushauri machache kuhusu maswali haya.
Soma Zaidi...Nitakujiza dawa ya chango na maumivu ya tumbo lahedhi, dalili zake na njia za kukabiliana na maumivu ya tumbo la chango.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maumivu wakati wa hedhi, haya ni maumivu ambayo utokea wakati wa hedhi kwa wanawake walio wengi, wengine huwa hawayapati kabisa na wengine hutapata na kwa kiwango kikubwa kutegemea na matatizo mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...