Posti hii inahusu zaidi malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba, ni malengo ambayo yametolewa ili kuweza kusaidia mtoto azaliwe vizuri na mambo mengine kama tutakavyoona.
Malengo kwa akina Mama na wachumba kabla ya kubeba mimba.
1.Lengo la kwanza kabisa ni kuhakikisha kuwa Magonjwa hatarishi kwa Mtoto na Mama yanajulikana mapema na yanadhibitiwa mapema, kwa mfano Magonjwa kama vile Magonjwa ya zinaa na Maambukizi ya virus vya ukimwi, Magonjwa kama yanatibika watayatibu kama hayatibiki dawa maalum zitatolewa ili kumkinga Mama na mtoto.
2.Kuhakikisha kwamba Mama anakuwa na vitu vyote muhimu ki afya kwa ajili ya yeye na mtoto kwa mfano kuwa na damu ya kutosha, vitamini za kutosha,kubwa na madini ya kutosha, mwili kuwa na kinga ya kutosha na kutokuwepo kwa magonjwa hatarishi ya kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto.
3.Tunafanya hivyo ili kumpa Mama elimu kama vile kuepuka mambo hatarishi kabla ya kubeba mimba kama vile matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya vileo vikali, matumizi ya madawa ya kienyeji, kuishi kwenye sehemu za viwanda vyenye kemikali kali, kutumia vitu vyote vyenye mionzi, kuwa na mazoezi yanayozidi mipaka kwa kufanya hivyo tutamwandaa mama ili aweze kupata mtoto asiye na Magonjwa.
4.Kwa hiyo basi tunapaswa kuwaelimisha wachumba wote na akina Mama wanaoendelea kuzaa wajiandae mapema ili kuweza kuepuka matatizo ya kupata watoto wenye ulemavu na Magonjwa ambayo yatawatesa katika maisha pale wazazi wanapoangaika ili kumtibisha mtoto na hatimaye kusababisha uchumi wa familia kushuka kwa hiyo tuendelee kutafakari msemo huu ambao unasema usipoziba ufa utajenga ukuta kwa hiyo wapendwa maandalizi ni ya muhimu sana na tunaokoa mambo mengi sana.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi njia za kutibu mbegu dhaifu, ni njia ambazo utumika kutibu mbegu ambazo ni dhaifu ili kuweza kuondoa tatizo hili ambalo limewakumba wanaume wengi na kusababisha madhara makubwa kwenye ndoa au familia.
Soma Zaidi...Nini humaanisha kama chuchu zinauma na hupati period mwanaidi mrefu.
Soma Zaidi...Download Kitabu cha elimu ya Ujauzito na malezi ya mimba.
Soma Zaidi...Posti hii utakwenda kutoa sababu kuu za kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi. Kama na wewe numiongini mwaka endelea kusoma
Soma Zaidi...Nimesoma makala yenu, sasa nina swaliJe kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Soma Zaidi...Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini.
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...