Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito



KUSHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI WA UJAUZITO




Hili ni swali ambalo wengi ya wajawazito wanajiulizaga. Kwa ufupi hakuna shida yeyote kushiriki tendo la ndoa wakati wa ujauzito, bila kujali hatua ya ujauzito. Unaweza kuzungumza na daktari kuhusu swala hili, ila usiwe na shaka kabisa. Tafiti zinaonyesha kuwa endapo mwanamke akifika kileleni akiwa katika ujauzito ni jambo jema kwa afya yake na afya ya mtoto na afya ya ujauzito. Najuwa maneno haya machache hayawezi kumaliza kiu ya maswali yako. Sasa hebu tuone mabo kadhaa.



1.Kwa baadhi ya wanawake wanapata maumivu wanaposhiriki tendo hili wakiwa wajawazito. Yes hii huweza kutokea kwani kzunguruko wa damu umeongezeka maeneo ya chini na kufanya maeneo hayo yawe na hisia nyingi sana. Hii inaweza kuleta hali ya kuumia kwa mjamzito wakati wa kuingia kwa uume. Wajitahidi wakati wa tendo hili kutumia muda mwingi kujiandaa, pia spidi upungue, na tendo lisifanyike kwa nguvu kama siku za kawaida.



2.Kuna baadhi ya wanawake wanajikuta uke wao umepunguza hali ya kubana yaani wanahisi unabwebwea. Ukweli ni kuwa kutokana na ongezeko la majimaji mwanamke anaweza kuhisi kuwa ule mnato na msuguano aliouzoea haupo. Hali hii inaweza kuwapunguzia hamu ya tendo baadhi ya wanawake.



3.Kwa baadhi ya wanawake majimaji yanakuwa mengi kiasi cha kuhisi kumkosesha raha mwenziwake. Hii hutokea baada ya msisimko kuzidi ama kwa sababu kuna mabdiliko ya homoni. Kama hali ni hii hakuna budi kuvumiliana.



4.Mkao wowte unaweza kutumika maadamu hautakandamiza tumbo la mama. Hapa wawe makini sana hasa ujauzito ukiwa mkubwa wasijelibana tumbo. Mkao wa ubavu ubavu na inayofanana na namna hiyo inaweza kuwa ni mizuri. Zungumza na daktari atakupa maelekezo vyema



5.Je kushiriki tendo kunaweza kusababisha ujauzito kutoka? Hapana si kweli kabisa. Ujauzito hauwezi kutoka eti kwa kushiriki tendo la ndoa.



6.Baada ya kushiriki tendo la ndoa kwa mjamzito anaweza kuona damu ama kutokwa na damu. Hii pia sio tatizo. Ila kama itakuwa inatoka kwa wingi vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.



7.Kwa baadhi ya wanwake inafikia wakati hahisi chochote anaposhiriki tendo na anakosa hamu kabisa ya kushiriki. Hili sio tatizo kubwa anaweza kumuona daktari kwa maelezo zaidi.



8.Kama atahisi dalili zifuatazo ni vyema kumuona daktari:
A.Maumivu makali zaidi yasiyovumilika
B.Damu nyingi
C.Kushindwa kupumuwa vyema



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 4229

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Wanaopasawa kutumia PEP

PEP Ni dawa ambazo utumiwa na watu wanaojamiiana na watu wenye virus vya ukimwi ila wenyewe hawawezi kupata kwa sababu ya kutumia dawa hizo.

Soma Zaidi...
Njia za kuongeza nguvu za kiume

Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume

Soma Zaidi...
Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi.

Soma Zaidi...
Je mwanamke anaweza pata mimba ikiwa wakati watendo la ndoa hakukojoa Wala kusikia raha yoyote ya sex wakati watendo landoa

Je wewe ni mwanmake unayepata shida kufika kileleni? (Kukojoa wakati wa tendo lwa ndoa). Post hii itakujibu baadhi ya maswali yako.

Soma Zaidi...
Kujaa gesi tumboni

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon

Soma Zaidi...
Endapo nina dalili za mimba na nikipima sina mimba, je, tatizo ni nini?

dalili za mimba zinaweza kuwa na mkanganyiko kwani zinafanana na shida nyingine za kiafya. Hali hii utaigunduwa endapo utakuwa na dalili za mimba lakini kila ukipima hakuna mimba.

Soma Zaidi...
Upungufu wa homoni ya estrogen

Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili.

Soma Zaidi...
Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.

Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano.

Soma Zaidi...
CHANGAMOTO ZA UJAUZITO, NA DALILI ZAKE NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO

Utawezaje kukabiliana na changamoto za ujauzito, je ni zipi changamoto hizo. Hapa nitakujuza.

Soma Zaidi...