Yajue mazoezi ya kegel

Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.

Faida ya mazoezi ya kegel.

1. Ni Mazoezi ambayo lengo lake kuu ni kuimarisha mifupa ya kwenye kiuno ambayo ushikilia kizazi hasa hasa mji wa mimba, kibofu cha mkojo, sehemu ya utumbo mpana na uke, kwa ujumla mazoezi haya huwa na faida zaidi kwa wanawake.

 

2. Lengo la mazoezi haya ni kuimarisha misuli kwa sababu misuli ya kwenye kiuno inaweza kuwa midhaifu kwa sababu ya ujauzito ila kama mtu anapiga mazoezi haya misuli hii uimarika kabisa na pia ikitokea mtu anafanyiwa upasuaji kama hapo mwanzoni alikuwa anafanya mazoezi haya ni rahisi kabisa kupona haraka.

 

3. Pia mazoezi haya usaidia kuimarisha njia ya mtoto wakati wa kujifungua kwa hiyo Mama kwenye kipindi cha ujauzito akifanya mazoezi haya ikifungua vizuri na mapema , kwa hiyo akina mama wanapaswa kujifunza mazoezi haya.

 

4. Usaidia pia wanawake wenye shida ya kuzuia mkojo kutoka, kuna wakati mwingine mkojo utoka kwenye kibofu bila mama mwenyewe kutoa mkojo huo na kwa hiyo kama mazozi haya yakifanyika vizuri na kwa usahihi yanasaidia akina mama kuweza kuhimili na kuzuia tatizo hili lisitokee.

 

5. Uongeza msisimko wa raha ya mapenzi kwa wapenzi wawili kwa mwanamke uweza kubana misuli ya kike  kwa umahiri zaidi wakati wa tendo usaidia wapenzi kufurahia tendo.

 

6. Kwa hiyo akina mama na wadada wanapaswa kujitahidi kufanya mazoezi haya ili kuweza kuhimalisha viungo vya uzazi ili wakati wa kujifungua iwe rahisi kwao na waepuke na matatizo mbalimbali yanayohusiana na uzaziJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/05/Sunday - 02:35:16 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1212


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-