Sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa


image


Posti hii inahusu zaidi sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa, Mgonjwa akiwa anaumwa na pia anakula chakula ni lazima asafishwe kinywa Ili kuweza kuepuka madhara mengine yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kinywani.


Sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa.

1.Tunamsafisha Mgonjwa kinywa ili tuweze kusafisha mdomo na meno kwa sababu kuna baadhi ya masalia ubaki mdomoni pindi tunapimlisha mgonjwa na pia kufanya meno ya mgonjwa juwa safi.

 

2. Tunamsafisha mgonjwa kinywa ili kuweza kuzuia kuaribika kwa meno na pia kuzuia maambukizi zaidi ya meno kwa sababu kuna vyakula vingine vinakuwa na sukari kwa hiyo vikikaa kwa mda bila kusafishwa Mgonjwa anaweza kupata Maambukizi kutokana na uchafu au meno kuoza.

 

3. Kuongeza mzunguko wa damu kwenye sehemu za kinywa, kama kuna uchafu ni vigumu damu kuzunguka kwa urahisi ila kama hakuna uchafu damu inaweza kusafili kwa urahisi kwenye kinywa cha mgonjwa.

 

4. Pia tunamsafisha Mgonjwa kinywa ili aweze kuwa huru na kuzuia harufu mbaya kwenye mdomo kwa hiyo kinywa likiwa kisafi na hamu ya kula ya mgonjwa uongezeka na pia katika kumfanyia mgonjwa usafi kinywani tunaweza kuondoa mabaki kinywani mwa mgonjwa.

 

5.Kwa hiyo tunapaswa kuwahudumia wagonjwa wetu vizuri na kuwaweka kwenye hali ya usafi kwa sababu na wenyewe wana hamu ya kuwa safi kwa hiyo tukiwa na wagonjwa nyumbani tuwahudumie na kwa kufanya hivyo tunaweza kuepusha hatari mbalimbali.



Sponsored Posts


  đꑉ    1 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       đꑉ    2 Madrasa kiganjani offline       đꑉ    3 Jifunze Fiqh       đꑉ    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Njia za kupambana na saratani
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani Soma Zaidi...

image Umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni mwa mama
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa maji yaliyomo kwenye mfuko wa mtoto akiwa tumboni. Ni maji ambayo kwa kitaalamu huitwa (Amniotic fluid) Soma Zaidi...

image Vyakula vya vitamini na faida zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake Soma Zaidi...

image Sababu za mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu.
Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine. Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa Uvimbe kwenye ubongo
Posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe au puto katika mshipa wa damu kwenye ubongo. Uvimbe kwenye Ubongo unaweza kuvuja au kupasuka, na kusababisha kuvuja damu kwenye ubongo. Mara nyingi, kupasuka kwa Uvimbe wa Ubongo hutokea katika nafasi kati ya ubongo na tishu nyembamba zinazofunika ubongo. Aina hii ya Kiharusi cha kuvuja damu huitwa Subarachnoid hemorrhage. Soma Zaidi...

image Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa Mama
Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama, tunajua wazi kubwa kuna faida kubwa za uzazi wa mpango kwa akina Mama pindi watumiapo njia hizi kwa uhakika zaidi. Soma Zaidi...

image Yajue magonjwa ya jicho
Posti hii inahusu zaidi Magonjwa ya jicho,ni Magonjwa ambayo ushambulia sehemu mbalimbali za jicho kwa mfano kwenye retina,kuaribu mishipa ya retina ,macho kuwa makavu na pia mtoto wa jicho, hali hii ya magonjwa ya macho Usababisha madhara mbalimbali kama vile kushindwa kuona vizuri, kushindwa kuona mbali au karibu,na hata Magonjwa haya yasipotibiwa uweza kuleta upofu. Soma Zaidi...

image Yanayoathiri afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayoathiri afya Soma Zaidi...

image Imani potofu kuhusu madawa ya hospitalini
Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu madawa yanayotolewa hospitalini, ni imani waliyonayo Watu hasa Watu wa bi vijijini na hata wa mjini nao wameanza kutumia madawa ya miti shamba kwa wingi. Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa kuungua Mdomo (mouth burning syndrome)
Ugonjwa wa mdomo unaoungua ni neno la kimatibabu kwa ajili ya kuwaka moto mara kwa mara mdomoni bila sababu dhahiri. Usumbufu huo unaweza kuathiri ulimi wako, ufizi, midomo, ndani ya mashavu yako, paa la mdomo wako au maeneo yaliyoenea ya mdomo wako wote. Ugonjwa wa mdomo unaoungua hutokea ghafla na unaweza kuwa mbaya. Soma Zaidi...