Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Ishara na Dalili za jeraha la jicho.
1. Kuwa na Maumivu kwenye jicho.
2. Uwekundu na uvimbe kwenye jicho.
3. Kutokuwa na uwezo wa kufungua jicho.
4.Kuwashwa kwa jicho
5. Kupungua kwa uwezo wa kuona
6.jicho kutoa machozi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walio na majeraha ya macho yaliyoingiliwa na uchafu Kama vile wadudu,kijiti,n.k
1. Mwambie mgonjwa aketi chini kwenye kiti anyanyue kichwa juu aangalie mwanga.
2. Simama nyuma ya mgonjwa ili iwe rahisi kumtoa uchafu Tumia Kidole gumba , kwa upole, tenganisha kope na uchunguze kilichopo ndani ya jicho.
3. Mwambie mgonjwa aangalie kushoto, kulia, juu na chini.
4.mwagia macho maji Safi na salama.
5. Ondoa kwa kutumia pamba au kitambaa Safi ili kuondoa uchafu.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanayohusiana na kemikali iliyomwagika kwenye jicho.
1. Ondoa mgonjwa kutoka eneo hilo, funga chombo cha kemikali
2. Mwagilia jicho la mgonjwa kwa maji baridi ya bomba kwa angalau dakika 10.
3. Usiruhusu maji yaliyochafuliwa kumwagika kwenye jicho ambalo halijaathirika
4. Mwambie mgonjwa atunze jicho lisilojeruhiwa kwa sababu Kuna uwezekano wa kuambikiza jicho lingine.
5 inapaswa utambue Ni aina ganu ya kemikali imeingia jichoni.
6. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanaliyoingiliwa na vitu vyenye ncha Kali Kama vile Pini,sindano,n.k
1. Weka kitambaa Safi juu ya jicho lililopata jeraha.
2. Mwombe mgonjwa atunze jicho lisilojeruhiwa kwa sababu harakati hii itasababisha msogeo wa jicho lililojeruhiwa ambalo linaweza kuongezea kupata Maumivu.
4. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi.
Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa wenye majeraha ya macho yanayohusiana na gesi
1. Hakikisha ulinzi wako mwenyewe kutoka kwa gesi
2. Mtoe mgonjwa kwenye Hilo eneo na kumweka sehemu yenye hewa nzuri.
3.mwambie mgonjwa kuwa atapona
4. Mkataze mgonjwa kusugua jicho
5. Mpeleke mgonjwa hospitali kwa usimamizi zaidi
Umeionaje Makala hii.. ?
Kama unahitaji kujuwa namna ya kuweza kujikinga na vidonda vya tumbo, basi makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utaweza kuzijuwa hatuwa zote za kujikinga na kupata vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kunywa pombe kiafya, ni madhara ambayo utokea kwa watu wanaokumywa pombe kwa kupita kiasi kwa hiyo wanapaswa kupunguza kunywa pombe baada ya kujua madhara yake.
Soma Zaidi...Katika vyakula tunaposema wanga tunamaanisha virutubisho ambavyo hupatikana kwenye vyakula. Hivi husaidia sana katika kuifanya miili yetu iwe na nguvu.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.
Soma Zaidi...Muulizaji anauliza he kula denda, ama kumbusu ama kufanya romance na muathirika was HIV na wewe uta ambukizwa?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hiii ni ratiba ambayo chanjo hii utolewa na ushauri mbalimbali utolewa ili kuweza kufanikisha kazi ya chanjo hii
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyekula chakula chenye sumu, kula sumu ni kitendo Cha kula kitu chochote kama dawa,pombe, kemikali na chakula kichafu.
Soma Zaidi...