Somo Hili linakwenda me kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara
.UVUTAJI WA SIGARA"uvutaji wa sigara ni hatari kwa afyaTafiti mbali mbali kuhusu sigara zinaonesha kuwa watu wameanza kuvuta sigara zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Historia zinaonesha kuwa misafara ya kibiashara na isiyo ya kibiashara imeshangia kueneza uvutaji wa sigara duniani. Inadaiwa cristopher columbas miaka ya 1492 aliwakuta watu maeneo ya America wakavuta sigara. Kutoka hapa sigara ikaenea maeneo ya ulaya kwa kupitia misafara hii.Mwanzoni iliaminika kuwa sigara hutibu baadhi ya magojwa. Dhana hii ilienea sana miaka ya 1600 ambapo watu wengi walijikita katika uvutaji wa sigara. Mnamo miaka ya 1800 viwanda vya kutengeneza sigara vilianzishwa japo sigara ilikuwa na bei kubwa.Miaka ya 1940 tafiti mbalimbali za kisayansi zilianzwa kufanya kuhusu sigara. Na hili lilitokea pale ambapo madaktari walipoanza kuhisi uhatari wa sigara kwa afya. Hapa wakaanza kuhusanisha sigara na saratani ya ini na mapafu. Mpaka kufikia miaka ya 1964 ripoti za kisayansi katika fani ya madaktari ziliwasilishwa marekani zikionesha uhatari wa sigara kwa afya ya watu.Kuanzia hapa maonyo mbalimbali yakaanzisha kuwaonya watu na uvutaji wa sigara. Kwanzia hapa ikaanzwa kukatashwa rasmi uvutaji wa sigara kwenye ndege, mikusanyiko ya watu, hospitali na maeneo mengine ya maofisi. Maonyo mengine yakawekwa kwenye pakti ya sigara.Sigara zinatengenezwa na tumbaku, huu ni mmea ambao unapatikana karibia dunia nzima. Tafiti za kisayansi zinaoneshakuwa tumbaku lina zaidi ya kemikali 400, ambapo nikotin ndio maarufu zaidi. Kwa ujumla kemikali hizi ni hatari kwa maisha ya mtu na afya ya jamii. Katika kemikali hizi nikotini ni sumu zaidi.Nikotini inapotumiwa huweza kuamsha mfumo wa neva, na kusababisha mapigo ya moyo kuenda kwa kasi zaidi. Nikotini ina hali ya kuwa addictive. Yaani mtu akisha izoea hawezi kukaa bila ya kuipata, nah ii ndio maana ni vigumu kuacha uvutaji wa sigara.Miongoni mwa hatari ambazo uvutaji wa sigara humletea mvutaji ni saratani ya mapafu. Tafiti zinzonesha kuwa sigara huenda ikawa ndio chanzo kikubwa cha saratani ya mapafu kuliko vyanzo vingine. Wavutaji wa sigara wapo hatarini kupata saratani ya mapafu kwa mara 20 zaidi ya wasiovuta. Pia sigara ni chanzo za aina zingine za saratani."hateful to the nose, harmful to the brain, and dangerous to the lungs." This was the view of England's king James I in 1604
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuzuia kiungulia
Soma Zaidi...Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari, ni wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi njia za kuenea kwa ugonjwa wa Ukimwi. Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa uterusi, ni mfuko unayosaidia kumtunza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukujuza kuhusu makundi manne ya damu, asili yake, maana ya antijeni na antibody, pia utajifunza kuhusu mfumo wa Rh. Mwisho utajifunza watu wanaopasa kutoa damu.
Soma Zaidi...Unapokuwa na kizunguzungu unashindwa kuudhibiti mwili wako, unaweza kuanguka kabisa.
Soma Zaidi...