Nyanja sita za afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu nyanja sita za afya
NYANJA SITA ZA AFYA
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Hata hivyo nadharia ya afya haiishii hapa ila inaendelea hata kujengwa katika mambo makuu sita. Mambo haya wataalamu wa afya wanayaita components of health. Mambo haya nitayataja hapa chini kwa ufupi tuu kama ifuatavyo
1.afya ya kimwili (physical health); hapa ni kuwa mzima kimwili, na afya hii huweza kujenga kwa kula vizuri, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Ukifanya hivi unaweza kuboresha mwili wako na kuboresha afya ya kimwili.
2.afya ya kiakili (mental health); hapa tunaangalia kuwa salama kiakili. Mtu akiwa na afya salama ya kiakili anakuwa na uwezo wa kujiamini, anapenda kujifunza vitu vivya na anavifurahia. Mtu mwenye hali hizi tunasema ana afya ya kiakili. Uwoga wa kuogopa watu ni katika maradhi ya kiakili.
3.afya ya mawazo na hisia (emotional health); hapa mtu anauwezo wa kuelezea hisia zake na mawazo yake. Kama kuna jambo limemuudhi analisema. Matu mwenye afya hii anauwezo wa kutaka msaada kwa mtu mwingine bia ya wasi.
4.Afya ya kiroho (spiritual health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na imani juu ya mambo fulani. Na mara nyingi hapa tunazungumzia kuwa na imani juu ya dini. Watalamu wa afya wanaonesha mahusiano makubwa kati ya dini na mtu. Wataalamu wanatuambia zaidi matu mwenye imani ya kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko mtu asiye na imani ya dini. -->
5.afya ya kijamii (social health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na mahusiano mazuri na jamii. Kusaidia watu, kuitikia watu wanapokuita na kucheka nao na kuzungumza nao ni katika mambo yanayojenga afya hii. Wataalamu wa saikolojia wanatueleza mengi kuhusu afya hii.
6.afya ya mazingira (environmental health); hii afya hujengwa na mazingira yanayotuzunguka. Mtu awe na uwezo wa kupata hea safi na maji safi. Hivi hujenga afya hii. Mazingira kuwa safi na salama huweza kutengeneza afyahii
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Jifunze jinsi ya kumsaidia mwenye kifafa
Kifafa hakiambukizi na ugonjwa wa ubongo lakini kifafa pia hakiathiri akili au ubongo Ila kikiwa kifafa Cha kudumu na Cha nguvu ndio huweza kuadhiri. Pia Kuna kifafa Cha mimba na kifafa Cha kawaida.kifafa Cha mimba ndio kinahatari Sana kuliko Cha Kawaid
Soma Zaidi...Faida za kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi faida za kusafisha vidonda, ni faida ambazo Mgonjwa mwenye vidonge uzipata kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Umuhimu wa uterusi
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa uterusi, ni mfuko unayosaidia kumtunza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA
Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.
Soma Zaidi...Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege
Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...