picha

Namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa

Posti hii inahusu namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa,ni njia unazopaswa kufuata wakati unamsafisha mgonjwa kinywa hasa wale walio mahututi.

Namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa kila mtu anaweza kuwa na mgonjwa kwa hiyo wagonjwa hao wanapaswa kufanyiwa usafi hasa wale walio mahututi na hawawezi kujifanyia usafi wenyewe kwa hiyo tunapaswa kufuata njia zifuatazo ili tusiweze kuleta madhara mengine kwa sababu pengine wanakuwa hawajiwezi hata kuongea hawawezi.

 

2. Kwanza kabisa  kama mgonjwa anaweza kusikia au kuongea ujamwambia unakuja kumfanyia nini kwa mda huo kusudi aweze kujua kinachoendelea.

 

3.Baada ya kumwambia unaosha mikono yako na unahakikisha kubwa unamjengaea mazingira ya kuwepo nyingi wawili yaani wewe na mgonjwa au na msaidizi wako kwa kufanya hivyo mgonjwa ataweza kuwaamini na kuwa huru ili umsafishe na sio kila mtu atakayepita ajue mnafanya nini.

 

4. Mwekee mgonjwa mto kwa nyuma na uso wake uangalie chini  ili kuhakikisha kuwa maji yanaweza kutiririka chini kwa urahisi kutoka mdomoni na hakikisha maji yasiingie kwenye mfumo wa hewa hasa kwa wagonjwa wale ambao hawajiwezi kabisa au hawawezi kuongea kabisa.

 

5. Weka kitambaa chini ili kuepuka kuchafua mashuka yaliyotandikwa, weka dawa ya meno kwenye maswaki, anza kumsafisha mgonjwa kwenye sehemu zote za kinywa sugua ulimi na fizi zote vizuri.

 

6.Suuza mdomo kwa kutumia maji safi kama mgonjwa hawezi hata kutema maji hakikisha unaruhusu maji yanamwagika kwenye beseni na ukitaka kuhakikisha kubwa maji yameisha chukua kitambaa kisafi na pangusa vizuri ili kuhakikisha kubwa maji yameisha ili yasije kuingia kwenye koo la hewa.

 

7.Baada ya kumaliza safisha vifaa vyote na virudishwe kwenye sehemu safi ili uweze kuvitumia tena

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/02/18/Friday - 11:43:33 am Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 1333

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEUNGUA

Kuungua kupo kwa aina nyingi.

Soma Zaidi...
Viwango vitatu vya kuungua.

Posti hii inahusu zaidi viwango vitatu vya kuungua. Ili tuweze kujua mtu ameunguaje Kuna viwango vitatu vya kujua kiasi na namna mtu alivyoungua

Soma Zaidi...
Madhara ya kunywa pombe kiafya

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kunywa pombe kiafya, ni madhara ambayo utokea kwa watu wanaokumywa pombe kwa kupita kiasi kwa hiyo wanapaswa kupunguza kunywa pombe baada ya kujua madhara yake.

Soma Zaidi...
Njia za kushusha presha

Post hii inakwenda kukujulisha njia za kushusha presha iliyopanda.

Soma Zaidi...
Madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu magonjwa ya vidonda vya tumbo, ni hatari inayotokea kwa mtu ambaye haujatibiwa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...
Huduma kwa watu waliodhani wamepatwa na maambukizi.

Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo utolewa kwa watu wanaodhani wamepatwa na maambukizi ya virus vya ukimwi.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu.

Soma Zaidi...
Chanjo zinazotolewa nchini Tanzania

Posti hii inahusu zaidi chanjo ambazo utolewa nchini Tanzania, ni chanjo ambazo uzuia Magonjwa ambayo yako katika sehemu mbalimbali za nchi.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa aliyeng'atwa na nyuki

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko

Soma Zaidi...