Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix.
Ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha.
1.Aina hii ya chanjo inazuia kuharisha kwa watoto na utolewa mara mbili na kwa vipindi tofauti tofauti pia uweza kutunzwa kwenye temperature kuanzia mbili mpaka nane na ikizidi au kupungua itaweza kuleta madhara na kwa ujumla isitumike, chanjo hiyo utolewa kwenye kinywa kwa miilis Moja nukta tano, na chanjo hii baada ya kutolewa uwa na madhara madogo madogo kama ifuatavyo.
2.Watoto wanaweza kukosa hamu ya kula,kuharisha na kutapika,joto la mwili kupanda na homa, maumivu ya tumbo na kuhisi uchovu wa mara kwa mara hasa kusinzia kwa mtoto na chanjo hii hapaswi kupewa mtoto mwenye mzio au aleji kwa hiyo hizo Dalili zikitokea na kuchukua mda zaidi ya masaa ishirini na manne mtoto anapaswa kupelekwa hospitalini ili kupata matibabu zaidi, ratiba ya chanjo ni kama ifuatavyo.
3.Chanjo ya kwanza unapaswa kutolewa kwenye wiki ya sita ambayo ni sawa na mwezi mmoja na wiki mbili, na kiasi ni sawa na mills moja nukta tano na pia utolewa kwa njia ya kinywa kwa hiyo ifikapo kila baada ya wiki sita walezi na wazazi wanapaswa kuwapeleka watoto kupata chanjo.
4.Chanjo ya pili inapaswa kutolewa baada ya wiki kumi ambazo ni sawa na miezi miwili na wiki mbili kwa hiyo ifikapo mda huu mama na walezi wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo na kiasi ni kile kile cha kwenye chanjo ya kwanza na daima upitishwa kwenye kinywa.
5. Kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka watoto kupata chanjo hii kwa sababu ina maana sana kwenye maisha ya watoto mbali tunajua wazi kuharisha kwa watoto ni hatari na upelekea maji kuisha mwilini na hatimaye mtoto anaweza kupata madhara makubwa zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyeungua na Moto.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na kumsaidia mwenye aliyeumwa na nyuki.nyuki na wadudu ambao wakikushambulia Sana na ukikosa msaada unaweza kufa au kuwa katika Hali mbaya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kizungu Zungu ni tatizo ambalo utokea kwa watu mbalimbali na kwa sababu tofauti tofauti na pengine mtu akipata kizungu sehemu mbaya anaweza kusababisha majeraha au pengine kupata ulemavu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida ya chanjo, tunajua wazi kuwa chanjo Ina faida kubwa kwenye mwili wa binadamu na vile vile kwenye jamii kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta
Soma Zaidi...