Maisha ya mtu yanaweza kuwa hatarini ama kupotea mara moja baada ya kunywa sumu.
Maisha ya mtu yanaweza kuwa hatarini ama kupotea mara moja baada ya kunywa sumu. Sumu inaweza kuwa katika vidonge, kimiminika, katika hali ya hewa ama kwenye sindano. Hapa nitazungumzia tu sumu inayoliwa na kuingia kwenye tumbo kwa njia ya mdomo. Sumu hii inawez akuwa ya panya am vidonge vya dawa.
Ukimuona mtu amekunywa ama kula sumu usimkimbie, na tambua kuwa anahitaji msaada wako. Kwanza angalia vyema hali yake na ukiwezekana ita msaada kwa haraka. Baad ya kufanya maamuzi kulingana na hali ya mgonwa unaweza kuanza kumpa huduma ya kwanza:
1.Mtapishe mgonjwa: kumtapisha mgonjwa ni katika njia nzuri na za haraka sana katika kupunguza athari za sumu. Unaweza kumtapisha mgonjwa kwa kumuingiza vidole mdomoni. Kama sumu ni ya kemikali mathalani amekunywa tindikali, njia ya kumtapisha sio njia sahihi.
2.Mpe maji mengi sana anywe. Kunywa maji mengi kutasaidia kupunguza makali ya sumu na kuiyeyusha kwenye maji.
3.Mpatie mgonjwa maziwa anywe. Unywaji wa maziwa uje baada ya kumtapisha. Usije mtapisha baada ya kumpa maziwa. Pia kama maziwa yapo usimpe maji mgonjwa.
4.Kama hali ya mgonjwa haijatengemaa, awahishe kituo cha afya kilicho karibu kwa haraka zaidi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Kuzimia ni hali ya kupoteza fahamu ambako kunaendana na kutokuhema.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu, madhara haya uwapata watu wengi kwa sababu hawajui taratibu za matumizi ya dawa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na shambulio la moyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli
Soma Zaidi...Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kupungukiwa damu mwilini, ni ugonjwa unaotokana sana hasa kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano ingawa na kwa watu wazima.
Soma Zaidi...Kama unahitaji kujuwa namna ya kuweza kujikinga na vidonda vya tumbo, basi makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utaweza kuzijuwa hatuwa zote za kujikinga na kupata vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...