Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho
17.Tango (coccumber).
Tango ni katika mimea jamii ya matikiti na maboga. Tango ni katika matunda ambayo unatakiwa uyale sana kwenye maisha yako. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia 95 ya tango ni maji. Tango lina vitamin K, B vitamins, copper, potassium, vitamin C, na madini ya manganese.
Tango lina anti-inflammatory flavonol ambayo huitwa fisetin. Hii husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo. Hii husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuimarisha afya ya mfumo wa fahamu pamoja na neva.
Tafiti zinaonesha kuwa tango lina polyphenols ambazo huitwa lignans (pinoresinol, lariciresinol, and secoisolariciresinol), husaidia katika kuzuia kupata aina mbalimbali za saratani (cancer) kama saratani ya kizazi kwa wanaume na wanawake.
Tango pia lina antioxidant flavonoids, kamavile quercetin, apigenin, luteolin, na kaempferol, ambazo husaidia katika kupambana na maradhi kama saratani na maradhi mengineyo.
Tango hupunguza joto tumboni, pia huondoa bajteria wanaoleta harufu mbaya mdomoni. Tafiti zinathibitisha kuwa tango husaidia katika kuondoa misongo ya mawazo na hii ni kutokana na uwepo wa vitamin B1, vitamin B5, and vitamin B7 (biotin) kwenye tango.
Tango huimarisha afya ya moyo na kupumguza shinikuizo la damu. Tanago husaidia mfumo wa kumengβenya chakula ufanye kazi kwa ufanisi. Tango husaidia katika kuthibiti uzito wa mwili.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula korosho
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu fati, vyakula vya fati, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za kula zabibu na umuhimu wake kiafya
Soma Zaidi...Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kutumia tangawizi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mchaichai
Soma Zaidi...