picha

Karanga (groundnuts)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga

. Karanga (ground nuts)

Karanga ni katika vyakula vya asili na ni kiungio cha mboga kwa jamii nyingi sana Tanzania na dunia kwa ujumla. Kama vilivyo vyakula vingine karanga ni katika vyakula vyenye virutubisho vingi. Ndani ya karanga kuna fotale, vitamin E, madini ya copper na arginine. Pia karanga ni chanzo kizuri cha omega-3 fatty acid, vitamin E na ijulikane kuwa fatty acid ni muhimu sana kwa afya ya moyo.

 

Ndani ya kjaranga kuna antioxidant iitwayo phenolic, polyphenol na resveratrol hizi husaidia katika kulinda mwili dhidi ya stress yaani misongo ya mawazo, na husaidia pia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani. Pia husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini yaani mfumo wa kupambamba na maradhi na mashambulizi ya magonjwa.

 

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina ya mafuta (fat) yaliyomo kwenye karanga ni mafuta ambayo ni salama kwa afya ya moyo. Kitaalamu aina ya fat iliyomo kwenye karanga ni monosaturated fat na polyunsaturated fat kwa ufupi fat hizi ni salama kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa usukiumwaji wa damu. Kwani fat hizi husaidia katika kupunguza cholesterol kwenye damu hivyo hupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo.

 

Karanga pia ni chanzo kizuri cha protini. Itambulike kuwa protini ni katika virutubisho muhimu na vinavyotakiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu. Seli za mwili zinahitaji protini kuweza kukuwa na kutengenezwa upya. Ukuaji wa mwili na uponaji wa vidonda na majeraha unahitaji protini.. watoto wanatakiwa wapewe vyakula vya protini kwa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha maendeleo ya ukuaji wao.

 

Tofauti na protini mwili unahitaji madini kwa kiwango kinachohitajika. Katika karanga kuna aina mbalimbali za madini kama vile magnesium, phosphorus, potassium, zinc, calcium na sodium. Madini yote haya husaidia katika ukuaji wa mwili na mwili kufanya kazi vyema.

 

Mafuta ya karanga yana fatty acid ambayo hutambulika kuwa inaongeza lipoprotein ndani ya mwili inayojulikana kama “good cholesterol” yaani cholesterol iloyo safi. Hii ni muhimu katika kuimarisha afya ya moyo na ubongo. Pia madini ya copper yaliyomo kwenye karanga husaidia katika kuzuia maradhi ya moyo yaani “coronary heart diseases”. pia vitamin B1 (thiamine) ni virutubisho muhimu katika kulinda mwili dhidi ya ufanyaji dhaifu wa kazi wa moyo. Yaani “cardiac failure”. na pia husaidia katika kuimarisha afya ya moyo.

 

Karanga husaidia katika kuboresha ngozi. Virutubisho vilivyomo kwenye karanga pamoja na vitamin C husaidia katika kuilinda ngozi dhili ya mikunjo mikunjo, madowa madowa na kuifanya ngozi iwe ang’avu, yenye majimaji na iyoyokuwa na ukavu au mikunjomikunjo. Uwepo wa anti-ageing phytohemical inayotambulika kama reseveratrol husaidia katika kumfanya mtu asizeheke kwa haraka.

 

Karanga husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa, kutokana na uwepo wa madini kama potassium, calcium, sodium, magnesium na phosphorus. Pia kwa wajawazito nivyema wakatumia chakula hiki kwani kuna protini na madini kwa ajili ya afya ya mama na mtoto

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views 2967

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Madhara ya upungufu wa protini mwilini

Madhara ya upungufu wa protini ni mengi kiafya. Miongoni mwa madhara hayo ni..

Soma Zaidi...
Faida za kula uyoga

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula uyoga

Soma Zaidi...
Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai

Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo.

Soma Zaidi...
Parachichi (avocado)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za parachichi

Soma Zaidi...
Vitamini C Ni nini?

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana na historia ya vitamin C

Soma Zaidi...
Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo, na vyakula salama kwa vidonda vya tumbo

Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Soma Zaidi...