faida za kula tunda zabibu kwa ajili ya afya yako
1.Zabibu (grapefruit).
Hili ni tunda ambalo lina historia kubwa kwenye maisha ya wanaadamu. Tunda hili linaweza kupatikana maeneo mengi duniani. Zabibu ni moja kati ya matunda yanayotambulika kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Afya ya mwanadamu tka zamani sana.
Zabibu linatambuliwa kuwa ni chanzo kizuri sana cha vitamini na madini kwenye miili yetu. zabibu ni katika matunda ambayo yana vitamini kwa wingi kuliko mengi katika matunda ambayo tunayala. Itambulike kuwa vitamini na madini ni katika virutubisho muhimu vinavyofanya mwili wako kuwa madhubuti na afya njema sikuzote.
Tunda hili pia hitambulika kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia kupunguza uzito wenye madhara mwilini mwako. Itambulike kuwa uzito ukizidi mwilini kuna matatizo mengi ya kiafya unaweza ukayapata kama kupata maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Hivyo tunda hili husaidia katika kupunguza uzito mwilini mwako. Ni vyema ukala tunda hili kabla ya kula chochote.
Tunda hili pia linatambulika kuwa na uwezo wa kusaidia kuweka madhubuti insulini iwe katika hali ya kawaidi. Itambulike kuwa insulin ikisumbua huweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Pia tunda hili husaidia katika kudhibiti afya ya figo. Kwa mfano zabibu hupunguza hatari za kupata maradhi ya figo yanayoitwa kidney stone yaani vijiwe vinavyokaa kwenye figo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kwa ufupi vyakula vya kuviepuka kama una presha ya kupanda.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza faida na matumizi ya asali mwilini.
Soma Zaidi...Post huu inakwenda kukupa orodha ya madini muhimu kwa ajili ya afya yako.
Soma Zaidi...Nashukuru kwa ushauri, Je!
Soma Zaidi...