Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma
Vitamini C ni katika vitamini ambavyo wili unavihitajia kwa wingi kwa lengo la kuboresha mfumo wa kinga mwilini. Tunaweza kupata vitamini hivi sana kutoka kwenye matunda. Katika makala hii nitakwenda kukutajia matunda aina 7 ambayo yana vitamini c kwa wingi sana.
Aina ya matunda yenye vitamini C
1.Embe, embe linafahamika kwa utamu wake na uchachu wake. Vitamini C vinapatikana kwa wingi zaidi kwenye matunda yenye uchachu.
2.Mapera; tunda hili limeenea maeneo mengi, kula pera likiwa limewiva ama likiwa limekomaa na tayari kulila.
3.Papai, mapapai ni katika matunda mabyo yana rangi ya njano. Matunda haya yana sifa ya kuwa na vitamini hivi kwa wingi
4.Karoti, kitaalamu karoti si tunda. Lakini nimependa kuliweka kwenye orodha hii kwa sababu watu hutafuna karoti na kuifanya kama tunda.
5.Limao na ndimu, hapa ndipo penyewe kwa vitamini C. limao na ndimu ndio matunda yenye uchachu kwa wingi na hivyo kukusanya vitamini C.
6.Nanasi, tunda hili pia ni katika matunda yenye rangi ya njano. Sifa hii hufanya tunda hili liwe miongoni mwa vyanzo vikuu vya vitamini C.
7.Chungwa, machungwa yana faida nyingi mwilini ikiwemo kutupatia vitamini C kwa wingi.
8.Nyanya, pensheni, palachichi, tufaha na pilipili haya ni katika matunda mengine yenye vitamini C kwa wingi kabisa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Zitambue aina zote za vyakule na ufanye maamuzi yaliyo kuwa sahihi katika uandaaji wa chakula chako
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi mbatata
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu upungufu wa protini na dalili zake
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula korosho
Soma Zaidi...Posti hii itakwenda kukupa faida za kula samaki kwenye mwili wako.
Soma Zaidi...