Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu
VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU
Damu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.
Kazi za damu mwilini
1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmengโenyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.
3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje
4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika
5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
Vyakula vya kuongeza damu mwilini
1.Nyama nyekundu kama nyama ya ngโombe, mbuzi. Kondoo
2.Maini
3.Nyama ya figo
4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi
5.Maharagwe
6.Kunde
7.Mayai
8.Nafaka nyinginezo
9.Njegere
10.Koeosho na karanga
11.Samaki
12.Nyama ya ndege
13.Karoti
14.Matikiti
15.Zabibu
16.Viazi vitamu
17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.
18.Polipili nyekundu
Dalili za kupungua kwa damu mwilini
1.Uchovu wa hali ya juu
2.Udhaifu wa mwili
3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko
4.Kupumua kwa shida
5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida
6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi
7.Maumivu ya kifua
8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi
9.Maumivu ya kichwa
Sababu za upungufu wa damu mwilini
1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6.Kuwa na maradhi ya sickle cell
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Vitamini C tunaweza kuvipata kwenye matuinda kama machunwa vina kazi kuu tatu ambazo ni hizi hapa
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina kuu tatu za vyakula na kazi zake, hii ni Aina tatu za vyakula na kazi zake jinsi zinavyofanya kazi, hufanya kazi kama ifuatavyo,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya Vitamini C, mwaka vilipogunduliwa na aliyegundua vitamini C
Soma Zaidi...Vitamini C ni moja kati ya vitamini muhimu sana katika kuboresha ufanyaji kazi wa mfumowa kinga mwilini yaani immune system. Katika post hii utakwenda kujifunza kazi za vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari.
Soma Zaidi...