Virutubisho vya mwili

Posti hii inahusu zaidi virutubisho vya mwili, ni aina tano za vyakula ambayo ufanya kazi mbalimbali kwenye sehemu za mwili wa binadamu.

Virutubisho vya mwili ni nini?

1.  Virutubisho vya mwili ni makundi yote matano ya vyakula yanayohitajika kwenye mwili wa binadamu Ili kuweza kurutubisha mwili, virutubisho hivi vimegawanyika katika makundi makuu matano ambayo ni wanga, kundi la pili ni protini, kundi la tatu ni vitamin, kundi la nne ni madini na kundi la tano ni maji, makundi haya matano kila kundi huwa na virutubisho tofauti tofauti ambavyo usaidia kujenga mwili.pia virutubisho hivi vina umuhimu mkubwa kwa watoto kama ifuatavyo.

 

2. Uongeza damu kwa watoto.

Tunajua wazi kuwa baadhi ya vyakula kama vile mboga mboga za majani na madini ya chuma usaidia kuongeza damu kwenye mwili kwa hiyo watoto ambao wameweza kula wanaweza kutumia mboga Ili kuepuka tatizo la kupungukiwa kwa damu.

 

3. Pia hivi virutubisho  uongeza hamu ya kula kwa watoto hasa hasa wale kwa wale watoto ambao hawapendi kula mpaka wakabwe, kwa hiyo tunajua wazi kuwa chakula ni dawa kwa hiyo katika chakula Kuna dawa ambayo usaidia kuwepo kwa hamu ya kula.

 

4. Vile vile virutubisho hivi uongeza uchangamfu kwa watoto waliozorota na kufanya mtoto awe na mwonekano Bora wa ki afya, kwa hiyo mtoto alichanganyiziwa vyakula mbalimbali uweza kuwa na virutubisho vyote vya mwili na kufanya awe na furaha kuliko kutumia aina Moja tu ya vyakula.

 

5. Huondoa unyafuzi na kiriba tumbo kwa mtoto.

Kuna watoto wengine ambao huwa na unyafuzi pamoja na kiriba tumbo hali hii uwapata kwa sababu ya kukosa vyakula vyenye mlo kamili kwa hiyo Akiongezewa vyakula mbalimbali anaweza kuwa na afya nzuri na mwonekano Bora.

 

6. Pia uondoa kudumaa kwa mtoto na kuongeza akili kwa mtoto.

Kwa kawaida tunajua wazi kuwa chanzo cha mtoto kudumaa na kuwa na akili ndogo usababishwa kukosekana na chakula Bora kwa wakati wa siku zake za mwanzoni, kwa hiyo mtoto akipewa vyakula mbalimbali na vilivyochanganywa vizuri na kwa wakati tofauti ana uwezekano mkubwa wa kutokudumaaa na kuwa na akili timamu katika makuzi yake.

 

7. Uweka kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Tunajua kuwa chakula ni dawa hasa hasa kama mtoto anakula vyakula mbalimbali na vyenye mchanganyiko mzuri na kwa mda tofauti na vilivyoandaliwa kwa usafi nakuhakikishia kuwa mtoto hawezi kupata magonjwa, kwa hiyo virutubisho kwenye chakula usaidia kukinga mtoto dhidi ya magonjwa.

 

8. Virutubisho kwenye mwili usaidia kufanya mwili watoto kuwa na mwonekano mzuri,kucha za mtoto kuwa nzuri pamoja na nywele za mtoto, hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa vyakula vya kujenga mwili kwenye chakula na kufanya sehemu za mwili za mtoto kuonekana safi kama vile ngozi, kucha na nywele.

 

9. Pia umfanya mtoto aweze kuona vizuri.

Kwa sababu ya kuwepo kwa vitamin mbalimbali kwenye vyakula hasa vitamin A umfanya mtoto aweze kuona vizuri, kwa hiyo ni vizuri kabisa kumpatia mtoto vyakula vyenye wingi wa vitamin A Ili aweze kuona vizuri.

 

10. Pia virutubisho kwenye mwili usaidia kuimarisha mifupa na meno kwa sababu ya kuwepo kwa madini mbalimbali kama vile calcium, kwa kula vyakula vyenye madini yanayoimarisha meno na mifupa usaidia kuepuka hatari ya kuwepo kwa matatizo ya meno na mifupa.

 

11. Upunguza sumu mwili kwa kuon doa antioxidant mwili  hivyo kupunguza kiasi cha macromolecules ambazo ni sumu kwenye mwili wa mtoto,kwa hiyo walezi wote na akina mama wanapaswa kuwapatia watoto vyakula mbalimbali vyenye mchanganyiko mzuri Ili kuweza kuepuka kuongeza kiwango cha sumu mwilini.

 

12. Pia virutubisho vya chakula mbalimbali uondoa tatzo la aleji au mzio kwa watoto kwa sababu ya kuwepo kwa mchanganyiko wa vyakula mbalimbali, kwa hiyo tuache tabia ya kutumia chakula cha aina Moja kwa watoto.

 

13. Pia usaidia mtoto apate usingizi mzuri kwa sababu ya kuwepo kwa dawa kwenye mchanganyiko wa vyakula ambazo uzuia matatizo ya kutopata usingizi.

 

14. Vile vile usaidia mtoto aweze kupata choo vizuri bila ya kuwepo choo kigumu au kuharisha kwa sababu ya kuwepo kwa mchanganyiko wa vyakula mbalimbali. Pia mchanganyiko wa vyakula mbalimbali uondoa homa kwa watoto.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 2427

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Namna ya kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba.

Posti hii inahusu namna au njia za kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba ya homoni imbalance kwa wanawake.

Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kula njegere

zijuwe faida za kula njegere kiafya na umuhimu wa kula jegere pia jifunze njegere zina kazi gani mwilini?

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA WANGA NA MADINI

Kuna aina nyingi za vyakula kama mafuta, wanga, fati, protini na vitamini. Je! unajuwa faida zake na hasara zake?

Soma Zaidi...
VYAKULA VYA VITAMIN NA MAJI

Zitambue aina zote za vyakule na ufanye maamuzi yaliyo kuwa sahihi katika uandaaji wa chakula chako

Soma Zaidi...
Rangi za matunda

Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo?

Soma Zaidi...
Vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito

Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito, mama mjamzito ni mama ambaye amebeba kiumbe ndani kwa hiyo anapaswa kutumia vyakula vyenye virutubisho mbalimbali vitakavyomsaidia mtoto kukua vizuri.

Soma Zaidi...
Fahamau protini na kazi zake, vyakula vya protini, na athari za upungufu wake.

unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo

Soma Zaidi...
Orodha ya madini, chanzo chake na faida zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake

Soma Zaidi...