Vyakula vya vitamini na faida zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake

VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKEVitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku.Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa, na mboga za rangi nya njano.. vitamin hivi ni muhimu kwa kusaidia afya ya macho na mfumo wa upumuaji (respiratory track). Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea mtu kushindwa kuona wakati wa usiku. Mwili unakuwa ni rahisi kupata mashambulio pindi mtu akiwa na vitamin A kwa uchache.Vitamin B1 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Husaidia katika kuhakikisha michakato ya kikemikali ndani ya seli inafanyika vizuri (metabolism). Pia husaidia katika kuunganisha taarifa za misuli. Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea ugonjwa wa beriberi ambopo mtu anakosa hamu ya kula. Misuli kukaza pia ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi. Wakati mwingine moyo kushindwa kufanya kazi ni kutokana na upungufu wa vitamin hivi.Vitamin B2 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Husaidia katika ufanyikaji wa michakato ya kikemia ndani ya seli (metabolism). Kupasuka kwa midomo ni dalili ya ukosefu wa vitamin hiviVitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele usio kobolewa na hamira.. huhitajika kwa ajili ya kuwasaidia enzymes kubadilimchakula kuwa energy. Pellagra ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa vitamin hivi. Mgonjwa anakosa hamu ya kula, misuli kukosa nguvu na kuharibika kwa ngozi.Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa na maini. Husaidia katika utengezaji wa damu, na utengezaji wa genetic meterials. Ugonjwa wa anaemia, upungufu wa uzito na nerve damage hutokana na upungufu wa vitamin hivi.Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Husaidia mwili kufyonza madini ya chuma. Kukosa nguvu za misuli,na maumivu ya viungio(joints)kutokwa na damu kwenye mafinzi kuchelewa kupona kwa vidonda na kuumwa mara kwa mara ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi.Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini. Husaidia katika kukuwa na kuimarisha meno na mifupa. Ugonjwa wa matege kwa watoto na osteoporosis yaani mifupa kuwa milaini husababishwa na upungufu wa vitamin D.Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na peanuts. Husaidi akatika kulinda utando uliopo ndani ya mwili. Mfumo wa fahamu kutokuwa katika hali ya kawaida ni dalili ya upungufu wa vitamin EVitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani. Husaidia katika kuganda kwa damu baada ya kupata jeraha. Damu kutoka kwa wingi baada ya jeraha ni upungufu wa vitamin K.Mtu atapata matatizo pia kama hata kunywa maji ya kutosha kwa siku. Maumivu ya kishwa huweza kusababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Choo kuwa kigumu huweza kusababishwa na uchache wa kunywa maji.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/11/11/Thursday - 12:15:15 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1466


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula panzi, senene na kumbikumbi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula panzi senene na kumbikumbi Soma Zaidi...

Faida za kula bamia
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula bamia Soma Zaidi...

Zijue Faida ya kula tunda la tango.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za kula tango japokuwa watu wengi hulipuuzia Ila Lina Faida kubwa Sana mwilini. Soma Zaidi...

Matunda yenye vitamin C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini na faida zake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake Soma Zaidi...

Faida za kula uyoga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula uyoga Soma Zaidi...

Faida za mbegu za maboga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mbegu za maboga Soma Zaidi...

FAIDA ZA KULA ZABIBU
Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za kula zabibu na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

Nyanya (tomato)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyanya Soma Zaidi...

je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?
Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo. Soma Zaidi...

Vitamini C Ni nini?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana na historia ya vitamin C Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula maboga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maboga Soma Zaidi...