(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w) :Ukiisoma Qur-an kwa makini utakuta kuna aya nyingi zinazojieleza kuwa Qur-an imeshushwa kutoka kwa Allah, kama inavyodhihirika katika aya chache zifuatazo:Lakini Allah anayashuhudia kuwa aliyokuteremshia (kuwa ni haki) ameyateremsha kwa ilimu yake, na Malaika (pia) wana shuhudia. Na Allah anatosha kuwa shahidi. (4:166).


"Uteremsho wa Kitabu hiki hauna shaka kuwa umetoka kwa Muumba wa ulimwengu. Je, wanasema: "Amekitunga mwenyewe ". (Sivyo hivyo). Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako ili uwaonye watu wasiojiwa na muonyaji kabla yako. Huenda wakaongoka." (32:2-3)


Na Kitabu tulichokuletea kwa wahyi ndicho cha haki, kinasadikisha (vitabu) vilivyokuwa kabla yake. Bila shaka Allah kwa waja wake ni Mwenye kuwajua vyema na kuwaona vizuri." (35:31)


Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule aliyeteremsha Qur-an kwa mja wake, ili awe muonyaji kwa walimwengu wote. (25:1)


Uteremsho wa Kitabu hiki umetoka kwa Allah, mwenye nguvu, na mwenye hikima. (45:2)Aya zote hizi na nyingi nyinginezo kama hizi zilizomo ndani ya Qur-an hujieleza wazi wazi kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w) alichowashushia wanaadamu kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Pangelikuwa na haja gani Mtume kuandika kitabu kisha adai kuwa kinatoka kwa Allah (s.w) tukikumbuka kuwa yeye amekuwa mwaminifu na mkweli katika historia yote ya maisha yake.