picha

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.

Sababu za kushuka kwa surat An-Nasr (idhaa jaa)

Sababu za kushuka surat an-Nasr (idhaa jaa)

SURATUN-NASR
Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.a.w) hupo maka wakati wa hija ya mwisho, hija ya kuaga. Sura hii matika mashafu imewekwa katika sura za Madina kwa sababu imeshuka wakati mtume ameshafanya hijira kwenda madina.



Sura hii inaitwa ya Madina kwa kuwa ilishuka baada ya Mtume kuhama ingawa iliposhuka ilikuwa ni katika Makka wakati Mtume alipokwenda kufanya Haji ya mwisho. Sura hii imekuja kutabiri kifo cha Mtume (s.a.w).



Kutokana na mapokezi ya hadithi sura hii ndiyo sura ya mwisho kushuka katika quran ila sio aya ya mwisho kushuka. Sura hii ilishuka kwenye masiku ya tashriq katika mwezi wa dhul-hija. Baada ya kushuka sura hii Mtume (s.a.w) ndipo akahutubia waumini.


Sura hii tukufu inaashiria kugomboka kwa Makka. Na sababu khasa iliyo pelekea kugomboka Makka ni Maqureshi walipo vunja mkataba wa amani wa Hudaibiya kwa kuwashambulia kabila ya Khuzaa', ambao walikuwa wana masikilizano na Mtume s.a.w., na wakawasaidia Bani Bakri katika hayo. Yalipo tokea hayo Mtume akaona waliyo yafanya Maqureshi kuvunja mapatano imembidi ende kuigomboa Makka. Basi akakusanya jeshi la nguvu lenye wapiganaji elfu kumi. Akenda mwezi wa Ramadhani katika mwaka wa nane wa Hijra (Desemba mwaka 630 B.K.) Akawazuia watu wake wasipigane ila wakilazimishwa. Na Mwenyezi Mungu alipenda aingie Nabii na jeshi lake Makka bila ya vita. Na kwa hivi akapata ushindi mkubwa kabisa katika taarikhi ya wito wa Kiislamu, bila ya vita. Na Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola ya kwanza duniani bila ya vita na bila ya kumwagwa damu.



Na huo ugombozi wa Makka ulikuwa na athari za kufikia mbali kwa pande za Dini na siyasa, kwani ilikuwa ni kuung'oa upagani, kuabudu masanamu, katika ngome yake kubwa, kwa kuvunjwa masanamu yaliyo simamishwa katika Al-kaaba, na yakaondolewa mapicha na masanamu yaliyo kuwemo.

Na kwa kuingia Makka kwenye boma la Uislamu Nabii s.a.w. aliweza kuzishinda kabila zote zilizo bakia katika Hijazi, ambazo zilizo kuwa zina kani za kijahiliya, kama Hawazan na Thaqif. Mwenyezi Mungu akamwezesha kusimamisha dola si juu ya kabila wala nchi bali juu ya Imani, nayo ni Imani ya Kiislamu, na bendera ya Kiislamu



Na Ushindi mkubwa uliotajwa hapa ni ushindi wa Makka ilipoingia katika mamlaka ya Waislamu, mwaka wa 8 wa Hijra, na mwaka uliofuata ikawa makundi-makundi ya makabila ya Waarabu yanakuja ingia Uislamu. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotimiza bishara Zake za ajabu; na Mtume s.a.w. anaambiwa aombe ghofira kwa ajili ya makundi hayo yatakayoingia Uislamu maana kazi ya kusimamisha sheria ilikuwa kubwa. Seyidna Abu Bakar iliposhuka sura hii alilia. Watu wakamwuliza mbona unalia? Akajibu, Kazi ya Mtume s.a.w. sasa imekwisha na Atatutoka.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views 3323

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka surat al adiyat

Sura hii iliposhuka ilikuwa kama imekuja kuwasuta Wanafiki waliokuwa wakizungumzahabari za uongo kuhusu jeshi alilolituma Mtume wa Allah.

Soma Zaidi...
Kulaaniwa Bani Israil

Pamoja na kuteuliwa na Allah(s.

Soma Zaidi...
ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN

ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.

Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat al qariah

Surat Al qariah, ni moja katika sura zilizochuka miaka ya mwanzoni mwa utume.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al Quraysh

Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.

Soma Zaidi...