Hukumu za kim sakina na tanwin ni idgham shafawiy, idh-har shafawiy, na Ikhfau shafawiy
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA :
Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Wataalamu wa tajweed wanataja hukuma zifuatazo kuhusu mym yenye sakina;-
i. إِدْغامُ الشَّفَ وِي Idghaam Ash-Shafawy
Hii hutokea pale ambapo miym yenye sakina ikukutana na miym yenye i’rabu yaani fataha, kasri au dhuma. Na inatakiwa mym yenye sakina ianze mwanzi kisha ifuatie mym yenye i’rabu, hivyo mym hii ya kwanza itaingizwa kwenye mym ya pili na kuwekwa shada ya pili na kusomwa kwa ghunnnah. Aina hii ya idgham pia huitwa إَدْغَامُ الْمُتَماثِلَيْن (Idghaamul-mutamaathilayni).
ii. إِخْ فَ اء الشَّفَ وِي Ikhfaaush-Shafawiy
Hukumu hii itapatikana pindi miym saakinah ( مْ) na herufi ya . ب, hivyo hapa mym sakina itafanyiwa ikhfaau kwenye ب, yaani mym ifafichwa kwa ghunnah.
iii. إظْهارُ الشَّفَ وي Idhwhaar Ash-Shafawiy
Hukumu hii hutokea wakati mym sakina inapokutana na herufi zozote isipokuwa م na ب, hivyoo hapa mym sakina itadhihirishwa yaani itatamkwa kama ilivyo pamoja na kuitenga na herufi inayofata bila ya kuleta ghunnah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Soma Zaidi...Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.
Soma Zaidi...Tafsiri ya quran kw akiswahili, imeandikw ana Shekh Ali Muhsin al-Barwani
Soma Zaidi...SURATUN-NASR Sura hii imeteremka wakati Mtume (s.
Soma Zaidi...Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran?
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...