(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.
(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.a.w):
Dai hili lilitolewa na Makuraishi katika enzi hizo za kushuka kwa Qur-an pia linaendelea kutolewa na makafiri wa karne hizi. Kwa mfano Stober, baada ya kusoma tafsiri ya Qur-an alidai kuwa itakuwa imeandikwa na Mwarabu ambaye ni mweledi wa historia ya Mayahudi na mila za nchi yake ambaye pia ni mshairi mzuri.
Udhaifu:
Wasomaji wa mashairi ya Kiarabu wanafahamu kuwa mashairi hayo yana mizani,beti na vina na yanaimbika kwa kiasi kwamba wakati mwingine inabidi hata maana au sarufi viwekwe pembeni alimradi tu shairi liimbike. Hivi sivyo kabisa ulivyo mfumo wa Qur-an. Qur-an si mashairi bali ni ujumbe wenye maana kamili ulioandikwa katika fasihi ya hali ya juu kwa kuzingatia sarufi na miiko yote ya lugha hai
.
Historia imeshuhudia kuwa Qur-an si mashairi. Ilikuwa kawaida ya washairi wakati ule wa Mtume (s.a.w) kubandika mashairi yao kwenye mlango wa Ka'aba kama changa-moto kwa washairi wengine. Ilitokea siku moja mshairi mashuhuri wa wakati huo, Labbiib ibn Rabiah, akabandika shairi lake kwenye mlango wa Ka'aba ili kutoa changamoto kwa washairi wengine. Shairi lake lilikuwa limetungwa kwa utaalamu mkubwa sana na lilikuwa zuri mno kiasi cha kutothubutu mtu yeyote kupambanisha shairi lake na hilo. Lakini baada ya kubandikwa kipande cha Sura ya Qur-an karibu na shairi lake, Labbiid mwenyewe (ambaye alikuwa Mshirikina) baada ya kusoma mistari michache ya sura hiyo alinaswa na mvuto wake na kuiamini dini iliyofunuliwa kutoka kwa Allah (s.w) na kubandua shairi lake
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu srat al fatiha, faida zake na maudhui zake
Soma Zaidi...Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.
Soma Zaidi...SURATUL-MAM’UUN Imeteremshwa Maka, anasimulia Ibn Jurayj kuwa Abuu Sufyan ibn Harb alikuwa na kawaida ya kuchinja ngamia wawili kila wiki, hivyo siku moja yatima mmoja alikuja kwake na kumlilia shida, na hakumsaidia kwa chochote na hatimaye akampiga yat..
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.
Soma Zaidi...