(vii)Mpangilio wa Qur-an:
Ukiuchunguza msahafu kwa kina utagundua kuwa si kitabu cha kawaida kama vile wanavyo vitunga wanaadamu. Qur-an pamoja na aya zake kufumwa na maneno ya Kiarabu, pametumika ujuzi usio na mfano katika uchaguzi na mpangilio wa maneno. Maneno yamechaguliwa na kupangiliwa kwa kiasi kwamba huwianisha habari zote zilizoelezwa ndani ya Kitabu na kuufikisha ujumbe kwa wepesi. Mifano michache ifuatayo itatupa picha ya mpangilio wa ajabu wa Qur-an:
Kwanza, kutokana na uchunguzi uliofanyika kwa kutumia kompyuta imedhihirika kuwa sura zile zilizoanza na herufi kama Qaf ( )zina idadi kubwa zaidi ya herufi hiyo ukilinganisha na herufi nyingine katika sura hizo.
Pili, Kuna sura 114 katika msahafu na kila sura imeanza kwa "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" isipokuwa Suratut Tawba. Hi huifanya idadi ya "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" kuwa 113. Lakini katika Suratun-Naml kuna "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" iliyoletwa katikati ya sura.
Imetoka kwa Suleimani, nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu,Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu." (2 7:30) Hivyo huifanya idadi ya "Bismillahir-Rahmaanir-Rahiim" kuwa 114 sawa na idadi ya sura zote katika msahafu. Je, hii imetokea kwa bahati tu au ni mpangilio wa Mjuzi, Mwenye Hikma.
Tatu, kutokana na uchunguzi imedhihirika kuwa maneno mbali mbali katika Qur-an yamerudiwa kwa kuzingatia idadi maalum. Kwa mfano neno "Sema" () limerudiwa mara 332 katika msahafu na neno "Alisema" () limerudiwa mara hizo hizo 332. Pia katika Qur-an zimetajwa "Mbingu Saba" ( ) na maneno haya yamerudiwa mara saba tu katika
msahafu mzima. Kuna miezi kumi na mbili katika mwaka mmoja na neno "Shahr"( )lenye maana ya mwezi limetajwa mara 12 katika Qur-an. Neno "Yaum" ( )katika Qur-an limetajwa mara 365 sawa na idadi ya siku za mwaka mmoja katika mwendo wa jua!
Nne, Qur-an inapofananisha jambo fulani na lingine, idadi ya utajo wa mambo hayo kitabuni humo pia huwiana. Kwa mfano katika sura ya 3 aya 59 Qur-an inasema: Bila shaka hali ya Issa mbele ya Allah ni kama ile ya Adam.Alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia kuwa na akawa. (3:59).
Adam(a.s) ametajwa mara 25 katika Qur-an. Issa(a.s) vile vile ametajwa mara 25 katika Qur-an. Zaidi ya hivyo katika sura 3:59, Adam ametajwa kwa mara ya saba vivyo hivyo Issa nae ametajwa kwa mara ya saba katika aya hiyo.
Adam(a.s) ametajwa katika aya zifuatazo:
2:31, 2:33, 2:34, 2:35, 2:37, 3:33, 3:59 (mara ya saba), 5:27, 7:11, 7:26, 7:31, 7:35, 7:35, 7:172, .17:61, 17:70, 18:50, 19:58, 20:115, 20:116, 20:117, 20:120, 20:121, 36:60.
Issa(a.s) ametajwa katika aya zifuatazo:
2:87, 2:136, 2:253, 3:45, 3:52, 3:55, 3:59 (mara ya saba), 3:84, 4:157, 4:163, 4:171, 5:46, 5:78, 5:110, 5:112, 5:114, 5:116, 6:85, 19:34, 33:7, 42:13, 43:63, 57:27, 61:6 na 61:14.
Mfano mwingine ni ule wa sura ya 7 aya ya 176. Qur-an inawalinganisha watu wanaofuata matamanio ya nafsi zao kinyume na aya za Mwenyezi Mungu, kuwa hao ni sawa na mbwa (Kalb).
"Hali yao ni sawa na ile ya mbwa:
Tamko:"Wale wanaokanusha aya zetu( ) limerejewa mara 5 katika Qur-an, na neno "mbwa"() limetajwa mara 5:
Tamko:"Wale wanaokadhibisha aya zetu limetajwa katika aya zifuatazo:7:176 (mara ya kwanza),7:177,21:77, 25:36 na 62:5 (mara ya tano).
Neno mbwa (kalb) limetajwa katika aya zifuatazo: 7:176 (mara ya kwanza), 18:18, 18:22
Aidha Qur-an inaposema jambo au kitu hiki si kama kile idadi ya mambo au vitu hivyo haiwiani katika kutajwa kwake ndani ya Qur-an.2
Kutokana na mifano hii michache ni muhali mwanaadamu kuweza kuandika kitabu chenye mfumo wa maneno, aya na sura mithili ya Qur-an.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 830
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Kitabu cha Afya
Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...
Sifa za waumini katika quran
Soma Zaidi...
Hukumu ya Ikhfau katika tajwid
Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid Soma Zaidi...
Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...
Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...
Sababu za kshuka surat al Asr
Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo… Soma Zaidi...
Maana ya qalqala na aina zake katika usomaji wa Quran tajwid
Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo. Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al humazah
Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka. Soma Zaidi...
Hukumu za Tajwid katika usomaji wa bismillah (basmalah)
Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah. Soma Zaidi...
Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake. Soma Zaidi...
Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Soma Zaidi...
Aasbab Nuzul surat Ash sharh: sababu za kushuka alam nashrah (surat Ash sharh)
Makala hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa alam nasharah yaani Surat Ash sharh. Soma Zaidi...