Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.
AL-IDGHAAM – KUINGIZA, KUCHANGANYA.
Idghaam ni kuingiza kitu kwenye kitu. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuingiza herufi saakin kwenye herufi yenye i’raab na kuzipelekea herufi mbili hizi kuwa herufi moja ya pili nzito. Na hutokea pale nuwn saakinah au tanwiyn inapofuatiwa na moja ya herufi sita za idghambazo ni ي ر م ل ن و
Sharti za idgham.
Idgham sikuzote inafanyika kwenye maneno mawili tu. Herufi ya mwisho ya neno la kwanza iwe na atnwiyn au nun sakina na herufi ya kwanza ya neno linalofata iwe ni moja ya herufi za idgham zilizotajwa hapo juu.
Sasa ikitokea nun sakina au tanwiyn zimekutana na moja ya herufi hizi za idgam katika neno moja hapa kinachotakiwa ni kuleta idhhar kwenye nun sakina au tanwiyn. Na hii idhwhaari ndiyo inayoitwa idhwhaar mutlaqa yaani idhwhaar halisi.katika qurani kuna maneno manne tu ambayo kuna idhwhaar mutlaqa.
Aina za idgham.
1.idgham bighunnah
Idghaam bighunnah ni kuingiza nuwn saakinah au tanwiyn kwenye herufi za ي ن م و pamoja na kuleta ghunnah inayotokea puani. Na hii hutokea pale nun sakina na tanwiyn zinapokutana na moja ya herufi hizo nne.
2.Idghaamu bighayri ghunnah
ة" إِدْغَامُ بِغَيْرِ غُن (Idghaamu bighayri ghunnah) ni kuitia na kuichanganya nuwn saakinah au tanwiyn katika herufi za ر ل bila ya kuleta ghunnah inayotokea puani.
Somo linalofuata utajifunza kuhusu makundi ya idgham.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.
Soma Zaidi...Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Soma Zaidi...