(vi)Kutokea Kweli Matukio yaliyotabiriwa katika Qur-an:
Ushahidi mwingine unaonesha kuwa Qur-an ni neno la Allah (s.w) ni kutokea mambo kama yalivyotabiriwa hapo awali na Qur-an. Katika mwanzo wa kushuka Qur-an kuna mambo mbali mbali ambayo Mtume (s.a.w) aliahidiwa pamoja na Waislamu kuwa yatatokea hapo baadaye. Pamoja na kuonekana kwa watu kutokuwa na uwezekano kutokea hayo yaliyotabiriwa kulingana na hali halisi iliyokuwapo wakati huo ukweli ni kwamba yalitokea. Kwa mfano, katika siku za mwanzo za Utume, Mtume (s.a.w) na Waislamu waliahidiwa na Allah (s.w) kuwa pamoja na ugumu uliokuwa ukiwakabili na pamoja na udhaifu wa mali na uwezo waliokuwa nao, hali yao itazidi kuwa nzuri siku hadi siku na baadaye watafarijika na kuwa juu ya maadui zao. Ahadi hizi tunazikuta katika aya zifuatazo:
Na bila shaka wakati ujao utakuwa ni bora kwako kuliko uliotangulia,na Mola wako atakupa mpaka uridhike. (93:4-5)
Na kwa hakika baada ya dhiki (huja) faraja. Hakika baada ya dhiki (huja) faraja. (94:5-6)
Tukiangalia maisha ya Mtume na maswahaba wake, ahadi zote hizi zilitimia. Waislamu waliongezeka siku hadi siku na Uislamu ulisimama na kuwa juu ya Dini zote (njia zote za maisha) katika kipindi kifupi cha miaka 23 tu.Mfano wa pili wa utabiri wa Qur-an uliotokea kweli baada ya kipindi kifupi tu ni ule uliotolewa katika suratur-Ruum katika aya zifuatazo:
Warumi wameshindwa katika nchi iliyo karibu (na nchi ya Bara Arabu, nayo ni Sham) nao baada ya kushindwa kwao watashinda, katika miaka michache: Amri hii ni ya Allah kabla (yake) na baada (yake) na siku hiyo Waislamu watafurahi kwa nusra ya Allah (Atakayowapa wao. Nayo ni kuwashinda Makuraishi siku hiyo) (Allah) Humnusuru amtakaye; naye ni Mwenye Nguvu; Mwenye Rehma. Hii ni ahadi ya Allah, Allah havunji ahadi yake lakini watu wengi hawajui. (30:2-6)
Katika mwaka wa sita au saba wa Utume, palikuja habari Makka kuwa Warumi ambao ni watu wa Kitabu (Ahlal-Kitab) wameshindwa vita na Waajemi ambao walikuwa ni washirikina kama washirikina wa Makka. Tukio hili liliwafurahisha sana washirikina wa Makka na kuwaambia Waislamu: "Wakristo, watu wa Kitabu kama nyinyi, wameshindwa na washirikina wenzetu, na hii ni ishara kuwa na sisi hivi karibuni tutakushindeni." Ndipo Qur-an ikatangaza katika aya hizi bishara mbili; bishara ya kwanza ni kuwa katika muda wa miaka tisa Waajemi watashindwa na Warumi na ya pili ni kuwa Waislamu siku hiyo nao watafurahi na kuwacheka Washirikina wa Makka, yaani makafiri wa Makka nao watashindwa vibaya sana na Waislamu. Hivi ndivyo ilivyotokea, kwani katika mwaka 624 A.D. Warumi waliwashinda Waajemi na mwaka huo huo Waislamu 313 walishinda jeshi la makafiri wa Makka lililokuwa na askari 1000 katika vita vya Badr, kwa hiyo ahadi ya Allah(s.w) aliyoitoa katika Qur-an ilitimia. Je hii haithibitishi kuwa Qur-an ni maneno ya Allah (s.w), Mjuzi wa yote yaliyopita na yajayo?
Hebu tuangalia tena mfano mwingine unaoonesha kutokea kweli ahadi alizozitangaza Allah(s.w) katika Qur-an. Katika suratul-Fat-h tunafahamishwa:
Bila shaka Tumekwisha kupa kushinda kuliko dhahiri. (48:1)
Katika mwaka wa 6 A.H. Mtume (s.a.w) na baadhi ya Maswahaba wake walitoka kwenda Makka kufanya Umra (Hija ndogo) lakini walipokaribia kuingia Makka makafiri waliwakatalia kata kata wasiende kufanya ibada hiyo.
Waislamu walikasirika sana mpaka kukaribia kupigana ndipo Allah (s.w) akawateremshia utulivu na wakakubaliana kufanya mkataba wa (Hudaibiya), kisha Allah (s.w) akawaahidi kupata ushindi baada ya muda mfupi. Ndivyo ilivyotokea.
Baada ya miaka miwili tu, na baada ya makafiri wenyewe kuvunja ule mkataba wa amani, Waislamu waliuteka mji wa Makka na kuwa mwisho wa kuabudiwa miungu mingine pamoja na Allah(s.w) katika Nyumba Takatifu (Al-Kaaba) na katika muda mfupi huo watu wengi walisilimu. Je, kutimia kwa bishara hii ambayo iko wazi mno katika historia, haioneshi kuwa haikutolewa na yeyote ila ni yule mwenye elimu ya hakika juu ya yote yaliyopita na yajayo?
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid
Soma Zaidi...Kuwa na tamaa huhitaji vitu vya watu si jambo jema. Ila kama tamaa hii itakuhamasisha na wewe kutafuta kitu hicho, kwa uwezo ambao Allah amekupa bila ha kuvuka mipaka yake, hili sio tatizo. Sura hii itakufundisha mengi
Soma Zaidi...Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Soma Zaidi...SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s.
Soma Zaidi...Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina.
Soma Zaidi...SURATUL-KAFIRUN Imeteremshwa maka na inaelezwa katika sababu za kushuka kwake ni kuwa Kundi la makafiri lilimfuata mtume (s.
Soma Zaidi...