Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake
(i)Mtume Muhammad (s.
(i)Mtume Muhammad (s.a.w) Kutojua Kusoma na Kuandika:
Iwazi mno katika historia yake kuwa Mtume (s.a.w) hakujua kusoma wala kuandika. Ukweli huu wa historia unathibitishwa na aya za Qur-an zifuatazo:
"Sema (Wewe Nabii Muhammad): Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyinyi nyote, (Allah) ambaye ana ufalme wa mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila Yeye, Ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi mwaminini Allah na Mtume wake, aliye Nabii Ummy, (asiyejua kusoma wala kuandika), ambaye humwamini Allah na maneno yake na mfuateni yeye ili mpate kuongoka." (7:158)
"Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, ingekuwa hivyo wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki)." (29:48)
Sababu ya Mtume (s.a.w) kutojua kusoma wala kuandika imebainishwa wazi katika aya hii ya (29:48) kuwa angelijua kusoma na kuandika watu wakaidi wasio tayari kumwamini Mtume na kuamini Qu-ran kwa sababu si maneno ya Allah(s.w) bali ni maneno aliyoyatunga Mtume (s.a.w) au ni maneno aliyoyanakili kutoka kwenye vitabu vya kale au ni maneno aliyofundishwa na watunga mashairi mashuhuri na kuyanukuu kwenye kitabu. Mtume (s.a.w) angalijua kusoma na kuandika ingalikuwa vigumu sana kuonesha udhaifu wa madai haya.
Lakini kutojua kusoma wala kuandika kwa Mtume (s.a.w) kumewafanya wapinzani wengi wakose hoja ya uwazi ya kukataa kuwa Qur-an si Kitabu cha Allah (s.w).Hata hivyo, pamoja na ukweli wa historia kuwa Mtume (s.a.w) hakuwa ni mwenye kujua kusoma wala kuandika, walitokea watu waliojitia upofu na kudai kuwa Qur-an ni maneno ya Muhammad (s.a.w). Ili kuwahuzunisha na kuwaonesha kuwa ni waongo katika madai yao hayo, Allah (s.w) aliwawekea watu hao na walimwengu kwa ujumla changa moto ambayo tutaiona katika kipengele cha (ix).
Kwa hiyo Mtume Muhammad (s.a.w) kutojua kwake kusoma wala kuandika na bado akawasilisha kwa watu ujumbe mzito wenye hekima kubwa na wenye kumuongoza mwanaadamu kwa usahihi katika kila kipengele cha maisha yake, ujumbe ambao hapana yeyote anayeweza kuleta mfano wake ni ushahidi mkubwa kuwa Qur-an yote kama ilivyo ni maneno ya Allah (s.w).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Ni nini maana ya id-gham katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza kuhusu maana ya id-ghamu na aina zake.
Soma Zaidi...Sababu za kushuka surat al Mauun
Sura hii ni katika sura ambazo zinahitaji kusomwa kwa mazingatio sana. Wanaoswali bila ya kuzingatia swala zao, wameonywa vikali sana. Wanaowatesa na kuwanyanyasa mayatima wameonywa vikali. Wanaowanyima wenye haja na masikini huku wakiwakaripia nakuwasem
Soma Zaidi...Sababu za kushuka surat al alaqa
Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran.
Soma Zaidi...