picha

Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir

Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir

(c)Dai la Kufundishwa na Jabir na Yasir:



Makafiri wengine wanadai kuwa Mtume (s.a.w) alifundishwa na Jabir na Yasir waliokuwa watumwa kutoka Ethiopia (Uhabeshi) na wakasilimu mbele ya Mtume (s.a.w). Wanadai hivyo kwa kuwa bwana wao aliyekuwa akiwatesa sana kwa sababu ya kusilimu kwao alikuwa akiwapiga sana na kuwaambia: "Mnamfundisha Muhammad?" na walikuwa wakijibu "Kwa jina la Allah hatumfundishi bali ndiye anayetufundisha na kutuongoza".



Bila ya kuangalia majibu ya Jabir na Yasir, wameshikilia swali alilouliza bwana wao kuwa ndio ushahidi wao kuwa Mtume (s.a.w) alifundishwa Qur-an na watu hao.
Makafiri wengine wamedai kuwa Mtume (s.a.w) aliiandika Qur-an kwa kusaidiwa na Salman aliyekuwa Mfursi (Persian). Salman alikuwa Mzoroastian kabla ya kuwa Mkristo huko Sham (Syria). Baadaye Salman alisafiri kwenda Madina ambapo alikutana na Mtume (s.a.w) na kusilimu.



Madai haya ni dhaifu kwa sababu mbili. Kwanza, karibu theluthi mbili ya Qur-an ilishuka Makka kabla Mtume (s.a.w) hajahamia Madina ambapo alikutana na Salman. Pili, fasihi ya lugha iliyotumika katika Qur-an ni ya hali ya juu mno kiasi ambacho wanafasihi mashuhuri wa Kiarabu walijaribu kwa miaka mingi kuigiza Qur-an bila ya mafanikio yoyote, itakuwaje Mfursi awe ndiye aliyeiandika?



Madai haya yamerejewa kwenye Qur-an kama tunavyosoma katika aya ifuatayo:



"Na bila shaka tunajua kwamba wanasema:"Yuko mtu anayemfundisha," (lakini) lugha ya yule wanayemuelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni na hii (lugha iliyotumika katika Qur-an) ni lugha ya Kiarabu fasaha (bulbul)." (16:103)



Madai yote haya pamoja na madai mengine mengi ambayo yamekuwa yakitolewa katika muda wote wa historia tangu ishuke Qur-an mpaka hivi leo, ni madai dhaifu mno ambayo hayana ushahidi wowote wa kiakili au wa kihistoria kuwa mwandishi (mtunzi) wa Qur-an ni mwengine asiye kuwa Allah (s.w).



Historia ya Mtume (s.a.w) imeandikwa na kuhifadhiwa vema kuliko historia ya mtu yeyote ulimwenguni, lakini hatuoni katika historia hiyo mahali popote tunapofahamishwa kuwa alikaa kitako kwa mtu yeyote kujifunza chochote. Kwani kama Muhammad (s.a.w) angelikuwa amesoma kwa Makasisi na Mapadri wa Kiyahudi na Kikristo au kwa mtu yeyote yafuatayo yangelijitokeza.



(a)Muhammad (s.a.w) hangelificha kueleza hayo kwani alikuwa mashuhuri katika maisha yake yote kwa kuhubiri na kusema ukweli. Aliitwa As-swadiq - Mkweli.
Ndani ya Qur-an yenyewe yamezungumzwa mambo yake ya ndani lakini bado hakuyaficha bali aliyadhihirisha kama yalivyo.



(b)Hangelifundisha imani iliyo tofautiana sana na Ukristo na Uyahudi hasa kuhusu misingi ya dini hizo. Lakini imani ya Kiislamu ni mbali na ni kinyume kabisa na imani ya Kikristo na Kiyahudi.


(c)Yeyote yule aliyemfundisha angeliweza kuandika kitabu mfano wa Qur-an angalau sura moja. Lakini hakutokea mtu yeyote mwenye uwezo huo.



(d)Mayahudi ambao katika Qur-an wameitwa "Ahlul-Kitaabi" au wana wa Israil (Bani Israil) wamekuwa katika muda wote wa utume wake wakimhoji-hoji Mtume Muhammad (s.a.w) na kumcheza shere na walikuwa wakimficha Mtume vitabu vyao. Kunawezekanaje watu hawa kama ndio waliomfundisha Mtume Qur-an wawe wanamhoji hoji tena juu ya Qur-an? Kama wangalikuwa wamemfundisha Mtume chochote, kwa nini wasingelikuwa watu wa kwanza kutangaza kwa watu kuwa wao ndio waliomfundisha ili kuonesha uongo wa utume wake?



(e)Mtume Muhammad (s.a.w) asingelikuwa mkweli katika utume wake na mwaminifu katika kutoa ujumbe aliotumwa autowe kwa watu, wafuasi wake wasingelikuwa wanyenyekevu kwake kiasi hicho na wasingelijizatiti katika kusimamisha mafundisho yake kiasi hicho katika mazingira magumu ya kufa na kupona. Historia inaonesha kuwa Waumini waliomfuata hawakumsaliti hata chembe.



Qur-an Inasadikisha Ukweli:
Sifa ya Qur-an ni kuwa inasadikisha yaliyo ya kweli katika vitabu vilivyopita. Hivyo Muislamu anaweza kujua kwa urahisi kabisa lipi ni sahihi katika Biblia na lipi si sahihi. Lolote lililomo katika vitabu vilivyotangulia ambalo linawafikiana na Qur-an ni sahihi. Na lolote linalokwenda kinyume na Qur-an ni batili.



Jambo la kusisitiza hapa ni kuwa kuhusu vitabu vilivyotangulia Qur-an imevitaja kuwa ni Suhf, Zabur, Taurat na Injili. Muislamu anayevikana vitabu hivi katika asili yake anakoma kuwa Muislamu.


Kama tulivyokwishasema Biblia inavyo kwa uchache vitabu 66. Agano la Kale lina vitabu 39 na Jipya inavyo 27. Katika vile 39 vya Agano la Kale ni vitano tu ndivyo vinavyoitwa Taurati ya Musa.



Qur-an inapotaja Taurati haikusudii Biblia au vitabu 39 vya Agano la Kale wala hivyo vitano vinavyodaiwa kuwa viliandikwa na Musa. Qur-an imeitaja Taurati kama ni ufunuo kutoka kwa Allah. Lakini tunaona kitabu cha Mwanzo ambacho kina taarifa za zamani sana kabla ya yeye (Musa) kuzaliwa. Hatuna uhakika kama kitabu hicho cha Mwanzo ilikuwa ni sehemu ya ufunuo alioupata kwenye mlima Sinai.



Isitoshe nusu ya kitabu cha Kutoka inazungumzia habari za kutoka kwa Wayahudi Misri. Hayo pia yalitokea kabla ya Musa kupata Taurati. Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ambacho inadaiwa kiliandikwa na Musa kimeandikwa pia habari za kufariki kwa Musa:



Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo. Musa alikuwa mtu wa miaka mia na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka. Wana wa Israeli wakamwombolezea Musa katika uwanda wa Moabu siku thelathini; basi siku za maombolezo ya matanga ya Musa zikaisha. (Kumbukumbu la Torati 34:4-1 2)



Ni dhahiri kuwa upo wasiwasi kama Nabii Musa (a.s) ndiye mwandishi wa kitabu hiki kwa sababu asingeweza kusimulia habari ya kifo chake na matanga yake mwenyewe.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 2225

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

quran na sayansi

YALIYOMONENO LA AWALI1.

Soma Zaidi...
Ni zipi hukumu za nuni yenye sakina au tanwin?

Hapa utajifunza usomaji wa Quran pindi utakapokuta nuni yenyebsakina au tanwin

Soma Zaidi...
Kwa nini quran ilishuka kidogo kidogo?

Kuna sababu nyingi za kuonyesha umuhimu wa Quran kushuka kwa mfumo wa kidogo kidogo

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA QALQALA

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Aina za usomaji wa Quran

Je kuna aina ngapi zabusomaji wa Quran

Soma Zaidi...
Sababu za kushukasurat an Nasr

Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W

Soma Zaidi...
Aina za Madda twabiy kwenye usomaji wa Quran

Madda zimegawanyika katika maeneo makuu mawili ambayo ni madda twabiy na madda fariy

Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
Kulaaniwa Bani Israil

Pamoja na kuteuliwa na Allah(s.

Soma Zaidi...