Menu



Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:

(vii)Dai kuwa Muhammad (s.

Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:

(vii)Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:



Wako baadhi ya watu wanaodai kuwa Muhammad(s.a.w) aliitunga Qur-an ili awaunganishe na kuwakomboa Waarabu. Dai hili pia halina nguvu kwa sababu zifuatazo:



Kwanza, lau dai hilo lingekuwa la kweli basi hapana shaka kuwa Qur-an ingetia msisitizo mkubwa sana katika mada ya umoja na ukombozi wa Waarabu. Kwa hakika hakuna aya hata moja katika Qur-an nzima inayolingania umoja na ukombozi wa taifa la Kiarabu. Itayumkinikaje basi Muhammad (s.a.w) atunge Kitabu kwa lengo la kujenga utaifa wa Waarabu na kusiweko katika kitabu hicho hata aya moja juu ya suala hilo?



Pili, msingi wa umma (taifa) unaofundishwa na Qur-an umejengwa juu ya itikadi ya haki na Qur-an inapinga hisia zote za utaifa kwa kufuata misingi ya rangi au kabila. Kila anayekubali itikadi ya Uislamu anakubalika katika umma wa Waislamu bila ya kujali rangi au kabila, au damu. Umoja uliodhihiri Arabia baada ya kushamiri kwa Uislamu ulikuwa umejengwa juu ya misingi ya Uislamu na siyo utaifa wa Kiarabu.



Tatu, lau umoja wa Waarabu ungekuwa ndilo jambo lililomsukuma Muhammad (s.a.w) hapana shaka angekubali kuwa mfalme wa Waarabu ili atumie fursa hiyo kujenga umoja wa taifa la Waarabu. Lakini tunaona alikataa ufalme pale wakuu wa Kikuraysh walipotaka kumrubuni ili aache kuutangaza Uislamu.



Nne, zipo aya katika Qur-an zinazolikanusha dai hilo. Aya mojawapo ya Qur-an yasema:


"Na (kumbuka) Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Kwa hakika


Allah amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote)." (3:42)
Aya hii inamzungumzia Maryamu, mama yake Nabii Isa (a.s). Maryamu alikuwa ni Myahudi.Na Wayahudi walikuwa wanadharau Waarabu kuwa ni taifa duni. Muhammad (s.a.w) alikuwa ni Mwarabu na Qur-an imeshuka kwa lugha ya Kiarabu na watu wa mwanzo kusomewa hii Qur-an walikuwa Waarabu.



Swali ni hili: Ikiwa Muhammad (s.a.w) alitaka kukuza hisia za utaifa wa Waarabu vipi basi aweke katika Qur-an aya hii inayomsifu mwanamke wa Kiyahudi kuwa amechaguliwa, ametakaswa na kutukuzwa na Allah(s.w) kuliko wanawake wote? Kwa nini asimsifie mama yake au mwanamke mwingine yeyote wa Kiarabu?
Aya nyingine ni hii ifuatayo:


Enyi kizazi cha Israili (Mayahudi)! Kumbukeni neema zangu nilizokuneemesheni, na nikakutukuzeni kuliko viumbe wengine. (2:47)
Mifano hii yaonesha kuwa haiingii akilini kuwa Muhammad (s.a.w) awe ametunga Qur-an kwa lengo la kuleta umoja na utukufu wa taifa la Waarabu halafu ndani ya hiyo hiyo Qur-an akasifia kwa sifa za kipeo cha juu kabisa watu walio maadui wa Waarabu!




                   


Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 906


Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰2 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA
SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( Ω…Ω’). Soma Zaidi...

KISA CHA TEMBO KATIKA QURAN, KUHUSU ABRAHA KUTAKA KUVUNJA AL-KABA NYUMBBA YA aLLAH
KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji. Soma Zaidi...

quran na sunnah
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al bayyinah
Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane. Soma Zaidi...

Mpangilio wa quran ni wa kipekee na uliotumia ujuzi mkubwa
Soma Zaidi...

Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al-Falaq na surat an-Nas na fadhila za kusoma sura hizi
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS) Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s. Soma Zaidi...

Amri ya Kuchinja Ng'ombe
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr. Soma Zaidi...

Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Soma Zaidi...

Wanaadamu kushindwa Kuandika Kitabu Mithili ya Qur-an:
Soma Zaidi...