Saratul-humaza

Saratul-humaza

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Adhabu kali itamthubutikia kila mwenye kuramba kisogo, asengenyaye, msengenyaji.
  2. Ambaye amekusanya mali na kuihesabu (tu bila ya kuitumia katika njia za kheri).
  3. Anadhania kuwa mali yake itambakisha milele.
  4. Hasha! Bila shaka atavurumishwa katika (moto unaoitwa) Huttama.
  5. Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini (huo moto unaoitwa) Huttama?
  6. (Huo ni) moto wa Mwenyezi Mungu uliowashwa (kwa ukali bara bara).
  7. Ambao unapanda (mpaka) nyoyoni.
  8. Hakika watafungiwa ndani ya moto huo.
  9. Kwa manguzo marefu (ili wasiweze kutoka).

 

Mafunzo kwa Ufupi.

  1. Kusengenya ni katika makosa makubwa kabisa.
  2. Ni makosa makubwa kukusanya mali bila kuitumia katika njia za kheri.
  3. Matumizi mabaya ya ulimi na neema zingine hupelekea kwenye maangamizi na adhabu.
  4.  Matumizi mabaya ya ulimi kama fitna, uongo, usengenyi, n.k. huleta chuki, husda na mtafaruku katika jamii.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views: 2703

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 web hosting     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 ai web app     👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Hoja juu ya kukubalika hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maswali yanayohusu quran

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
quran na sayansi

YALIYOMONENO LA AWALI1.

Soma Zaidi...
Asbab nuzul surat at Tin, Sababu za kushuka surat at Tin (watin wazaitun)

Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun).

Soma Zaidi...