Lugha ya kiarabu Lugha ya quran: kwa nini quran katika lugha ya kiarabu

Lugha ya kiarabu Lugha ya quran: kwa nini quran katika lugha ya kiarabu

Lugha ya kiarabu Lugha ya quran: kwa nini quran katika lugha ya kiarabu

Lugha ya Qur-an:



Lugha iliyotumika katika Qur-an ni Kiarabu sanifu kama tu navyoj ifu nza katika Qur-an yenyewe:


"Na namna hii tumekufunulia Qur-an kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembezoni mwake. Na uwaonye siku ya mkutano, siku isiyo na shaka. Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jingine Motoni " (42:7)



Kwa nini Qur-an Imeshushwa kwa Lugha ya Kiarabu?
Walimwengu walio wengi wakiwemo baadhi ya Waislamu wanaitakidi kuwa lugha ya Kiislamu ni Kiarabu na Uislamu ni dini ya Waarabu. Bila shaka mawazo haya yamejitokeza kutokana na kutoujua Uislamu kwa upeo wake. Uislamu ni Dini ya Walimwengu wote wa nyakati zote na ni Dini iliyofundishwa na Mitume wote. Je, Mitume wote walikuwa Waarabu au watu wote waliolinganiwa na Mitume hao na kuwafuata walikuwa Waarabu? Bila shaka jibu litakuwa "hapana". Bali tunajifunza katika Qur-an yenyewe kuwa Allah (s.w) amewajaalia walimwengu kuzungumza lugha mbali mbali na ni katika ishara ya Uungu wake na utukufu wake.


"Na katika Ishara zake (zinazoonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi, na kuhitilafiana lugha zetu na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi." (3 0:22)


Kwa nini Qur-an imeshushwa kwa lugha ya Kiarabu? Jibu lake linapatikana ndani ya Qur-an yenyewe:


"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia. Kisha, Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye (kwa kuwa hataki kufuata ujumbe uliomfikia wazi wazi) na humuongoza amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Hekima." (14:4)



Aya hii inatufahamisha kuwa kila Mtume alishushiwa Wahyi kwa lugha ya watu wake ili yeye mwenyewe apate kuwabainishia vizuri na wao wapate kumuelewa vizuri. Kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu wa kabila la Kiquraishi na kwa kuwa Maquraish na Waarabu kwa ujumla ndio watu wake wa mwanzo kuwalingania Uislamu ili wamsaidie kuufikisha ulimwengu mzima. Qur-an ilibidi ishushwe kwa lugha ya Kiarabu cha Kiquraish kilichokuwa fasaha kuliko vilugha vyote vya Kiarabu. Watu wake wasingemuelewa kabisa kama Mtume (s.a.w) angewalignania kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu:


"Na lau kama tungaliifanya Qur-an lugha isiyo ya Kiarabu wangelisema: Kwa nini aya zake hazikupambanuliwa? Lo! Lugha isiyokuwa ya Kiarabu na (Mtume) Mwarabu! (Mambo gani hayo)? " (41:44).


"Na lau tungaliiteremsha juu ya mmoja wa wasiokuwa Waarabu, na akawasomea (kwa ufasaha) wasingalikuwa wenye kuamini." (26:198-199)


Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:
(i)Ni desturi ya Allah (s.w) kumtuma mjumbe wake kwa lugha ya watu wake anaowafikishia.
(ii)Qur-an imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu na wale aliowalingania mara ya kwanza walikuwa ni Waarabu.
(iii)Waarabu wa mwanzo kulinganiwa Uislamu na Mtume (s.a.w) wasingeliukubali ujumbe kama Mtume asingelikuwa Mwarabu na kama angelingania kwa lugha nyingine isiyokuwa ya Kiarabu.
(iv)Kama Mtume (s.a.w) angelingania kwa lugha nyingine isiyokuwa Kiarabu, ujumbe wake usingelifahamika na watu wake wasingelazimika kuufuata kwa kuwa hawauelewi.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views: 6857

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 ai web app     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Fadhila za kusoma surat al Baqarah

Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.

Soma Zaidi...
quran na tajwid

TAJWID Utangulizi wa elimu ya Tajwid YALIYOMO SURA YA 01 .

Soma Zaidi...
Tofauti kat ya sura za Maka na Madina

Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina.

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Fatiha (Alhamdu)

Post hii inakwenda kufundisha fadhila na faida za kusoma Alhamdu.

Soma Zaidi...