Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
SURAT AL-MUAWIDHATAYN (SURAT AL-FALAQ NA SURATUN-NAS)
Inaelezwa kuwa sura mbili hizi zilishuka pamoja, na maulamaa wanaelezea kuwa Mtume (s.a.w) alirogwa na wachawi wa kiyahudi kwa kutumia nywele zake kisha uchawi ule wakautumbukiza kwenye kisima cah Banu quraidha, na aliyewapa nywele wachawi hao ni labid ibn Aa€™swam. Mtume aliumwa kwa muda wa miezi sita iala uchawi huu haukuathiri akili yake. Hata sikumoja alipolala wakaja malaika wawili na mmoja wao akauliza kumuuliza mwenziwe ana nini huyu (Mtume) yule wa pili akajibu amerogwa kisha akaeleza namna alivyorogwa na mwisho akaeleza tiba ya uchawi ule ndipo akasoma sura mbili hizi. Na hii ndiyo husemwa sababu ya kushuka kwa sura hizi. Sura hizi zimeteremka madina.
FADHILA ZA SURA HIZI
Amesimulia ‘Abdallah Ibnhabib kuwa Mtume amesema “QUL HUWA LLAHU AHADU na mu’awadhatayn (qul a’udhu birabin-nasi na qul a’udhu birabil-falaq) (mwenye kuzisoma ) asubuhi na jioni zinatosheleza kwa kila kitu.(amepokea ahmad, Tirmidh na Nisai).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun).
Soma Zaidi...Sura hii ni katika sura ambazo zinahitaji kusomwa kwa mazingatio sana. Wanaoswali bila ya kuzingatia swala zao, wameonywa vikali sana. Wanaowatesa na kuwanyanyasa mayatima wameonywa vikali. Wanaowanyima wenye haja na masikini huku wakiwakaripia nakuwasem
Soma Zaidi...Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran.
Soma Zaidi...