picha

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)

(d)Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)


"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu ni kwangu, hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda." (31:15).



Aya inabainisha wazi kuwa hatupaswi kuwatii wazazi wetu pale watakapotuamrisha kumuasi Allah (s.w). Tukiwatii tutakuwa tumemshirikisha Allah (s.w) kwa kuwafanya wazazi wetu miungu badala yake kama inavyo bainika katika Qur'an.



“Mayahudi na Wakristo) wamewafanya wanavyuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allah (s.w) …." (9:31)



Iliposhushwa aya hii Adi bin Hatimu (r.a) ambaye alisilimu kutoka kwenye Ukristo, alimtaka Mtume (s.a.w) atoe ufafanuzi kwa sababu alidai kuwa kinadharia hawakuwa wanawafanya watawa wao miungu. Katika kufafanua, Mtume (s.a.w) alimuuliza Adi, "Je hawakuwa watawa wenu wanawahalalishia alivyo viharamisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii?" Alijibu Adi, "Ndiyo" Mtume (s.a.w) akamuuliza tena, "Je watawa wenu hawakuwa wanakuharamishieni alivyo halalisha Allah (s.w) na nyinyi mkawatii? Adi akajibu tena "Ndiyo." Basi Mtume (s.a.w) akasema, "Huko ndio kuwafanya miungu".



Hivyo, kumtii mzazi au kiongozi au yeyote yule katika kumuasi Allah (s.w) ni kumfanya mungu badala ya Allah (s.w). Pia ukitii matashi ya nafsi yako kinyume na amri au makatazo ya Allah (s.w) utakuwa umeifanya nafsi yako mungu badala ya Allah (s.w).


"Je, umemuona yule aliyefanya matamanio yake, (kile anachikipenda), kuwa Mungu wake? Basi je, utaweza kuwa mlinzi wake (ukamhifadhi na hayo, na hali ya kuwa hataki?). "(25:43).



Lakini, tunaamrishwa katika aya hii (31:15) kuwa pamoja na kutowatii wazazi wetu katika kumshirikisha Allah (s.w), tusiwe jeuri na fedhuli kwao, bali tuzungumze nao kwa upole kwa kauli njema na tuendelee kuwatii na kuwafanyia wema katika mambo yote ya halali.


Wakati mwingine wazazi wanaweza kutishia kuacha laana tutakapowakatalia kwa kauli nzuri kutowatii katika yale yatakayotupelekea kumuasi na kumshirikisha Allah (s.w). Tusiyumbishwe na tishio hili kwa sababu marejeo yetu sote ni kwa Allah (s.w) na ni mjuzi kamili juu ya dhamira (nia) zetu na vitendo vyetu - "…kisha marejeo yenu ni kwangu, Hapo nitakuambieni mliyokuwa mkiyatenda" (31:15).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 1903

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Dua za Mitume na Manabii     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 ai web app     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote

Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)

Soma Zaidi...
Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu

Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)

Soma Zaidi...
Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?

Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)

Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.

Soma Zaidi...
Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia

Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia.

Soma Zaidi...
Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali

Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.

Soma Zaidi...