Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;
Milango ya fahamu kama vile macho katika kumuona, pua katika kumnusa, masikio katika kumsikia, ngozi katika kumhisi au kumgusa pia, n.k.
Udhaifu wa hoja hii,
Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama upepo, sauti, n.k.
Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia muingu.
Udhaifu wa hoja hii,
Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake.
Rejea Qur’an (2:31,38).
Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na hatimaye mtu kamili.
Udhaifu wa hoja hii,
Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuthibitisha nadharia hii.
Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.
Udhaifu wa hoja hii,
Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu vyote. Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na vitu au maumbile yale.
Rejea Qur’an (112:1-4).
Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.
Udhaifu wa dai hili,
Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na kimewekwa kwa lengo maalum.
Makafiri wanadai kuwa kuamini kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) ni ububusa na kufuata mkumbo bila ya udadisi na kutumia akili. Dai hili sio la kweli kwa sababu zifuatazo;
Kwanza, Mwenyezi Mungu (s.w) ametuma Mitume mbali mbali kwa wanadamu ili kuwafundisha na kutoa dalili za kuwepo kwake bila ya shaka yeyote kwa dalili za wazi ili kumfahamu na kuweza kumuabudu ipasavyo.
Rejea Qur’an (4:165).
Pili, Vipawa, ufahamu na akili alivyopewa mwanaadamu ni kumuwezesha kumtambua Muumba wake na kuweza kumuabudu inavyostahiki. Hivyo kutotumia akili katika kumtambua Mwenyezi Mungu kupitia ishara mbali mbali ni kustahiki adhabu.
Rejea Qur’an (3:190), (30:21), (7:179), (8:22) na (12:105).
Tatu, Mitume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwafundisha wafuasi wao juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu, hawakuwataka kuamini na kufuata bila ya hoja na dalili za wazi bali walionyesha ishara na miujiza kuthibitisha ujumbe wao.
Nne, Msisitizo wa Elimu katika Qur’an kuwa faradhi ya kwanza kama nyenzo pekee ya kumuwezesha mwanaadamu kumjua na kumuabudu Mola wake na kuweza kuyamudu mazingira yanayomzunguka na kuweza kusimamisha Ukhalifa ardhini.
Tano, Maana ya neno “imani” ambalo lina maana ya ‘kuwa na yakini moyoni pasina shaka’ yeyote juu ya jambo fulani kwa kuwa na ujuzi nalo na pia kupitia dalili na ishara za kutosha za kuonyesha kuwepo kwake.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1229
Sponsored links
👉1
Madrasa kiganjani
👉2
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3
Kitau cha Fiqh
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Kitabu cha Afya
👉6
kitabu cha Simulizi
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu...
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...
Maana ya uislamu.
Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti. Soma Zaidi...
Sifa za wuamini zilizotajwa katika surat Al-ma'aarij
Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko. Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab
Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu. Soma Zaidi...
Mtazamo wa uislamu juu ya dini
Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini. Soma Zaidi...
KUAMINI SIKU YA MALIPO
Soma Zaidi...
mgawanyiko wa elimu
Soma Zaidi...
KUAMINI VITABU VYA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s. Soma Zaidi...
Kina Cha uovu wa shirk
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...