Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
- Baada ya kufanyiwa hatua hizo, sasa ni lazima maiti kufanyiwa yafuatayo:
- Mambo haya ni faradh Kifaya, wakifanya wachache wanawakilisha wengine.
- Kuoshwa (Kukoshwa).
- Mazingatio kabla ya kuosha maiti.
- Maiti ya kiume ioshwe na wanaume na maiti ya kike ioshwe na wanawake pia.
- Maiti ya mtoto yaweza kuoshwa na yeyote.
- Ni Sunnah mke kumuosha mumewe na mume kumuosha mkewe pia
- Ni mtu mmoja tu ndiye anayeosha na mwingine ni kwa ajili ya kumpa msaada inapobidi.
- Ni muhimu muoshaji afahamu masharti ya kuosha maiti muislamu kama vile;
- Muoshaji awe muislamu.
- Mahali pakuoshea pawe faragha (pamesitirika).
- Maiti aoshwe huku amefunikwa gubi-gubi na nguo nyepesi inayoruhusu maji kupenya kwa urahisi.
- Ni vyema muoshaji asiishike maiti bali aoshe akiwa amevaa ‘gloves’.
- Kuzingatia masharti ya mwenye kuoga josho la wajibu; kama vile kuwa na maji mengi na safi, pasiwe na kizuizi cha maji kupenya, n.k.
- Ni muhimu muoshaji afahamu nguzo na sunnah za kuosha maiti kama ifuatavyo;
- Nguzo za kuosha maiti ni mbili:
- Nia
- Kueneza maji mwili mzima wa maiti.
- Ni Sunnah kumuosha maiti mara tatu au zaidi kwa idadi ya witiri.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 ai web app 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Makundi ya dini za wanaadamu
Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu.
Soma Zaidi...Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera.
Soma Zaidi...Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali
Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.
Soma Zaidi...Nini chanzo cha elimu zote na ujuzi wote
Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Ni Ipi Elimu yenye manufaa
Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Soma Zaidi...