Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kucheza na data kuzibadili kwa namna mbali mbali kwenye template
Katika Django, templates hazitumiki tu kuonyesha data, bali pia zina uwezo wa kuchakata (manipulate) data moja kwa moja bila ya kuandika Python code kwenye views.
Hii huwezekana kwa kutumia:
✅ Template Filters – Zinawezesha kubadilisha maelezo kwa urahisi kama kubadilisha herufi kuwa kubwa/ndogo, kukata maandishi, n.k.
✅ Template Tags – Zinawezesha kutekeleza logic kama loops na conditions (maamuzi) ndani ya template.
Kupunguza mzigo kwenye views – Badala ya kufanya formatting zote upande wa Python, templates zinaweza kushughulikia mwonekano wa mwisho.
Kutenganisha logic na presentation – Logic ya data hubaki kwenye views wakati formatting inabaki kwenye template.
Urahisi wa kuhariri mwonekano – Mabadiliko madogo ya namna data inavyoonyeshwa hayaathiri view.
Filters hutumika kwa kutumia |
(pipe) ndani ya {{ }}
.
Muundo wa matumizi:
{{ variable|filter }}
{{ variable|filter:"arg" }}
Katika Django templates, kuna filters mbalimbali zinazotumika kubadilisha maandishi moja kwa moja bila kutumia Python code kwenye views. Moja ya filters maarufu ni upper
, ambayo hubadilisha herufi zote kuwa kubwa. Kwa mfano, {{ "jina"|upper }}
litatoa matokeo JINA
. Vilevile, filter ya lower
hubadilisha herufi zote kuwa ndogo, kama vile {{ "JINA"|lower }}
ambayo itatoa jina
.
Filter nyingine muhimu ni title
, inayofanya herufi ya kwanza ya kila neno iwe kubwa. Mfano {{ "python django"|title }}
litazalisha Python Django
. Ikiwa unataka kubadilisha tu herufi ya kwanza ya neno la kwanza, utatumia capfirst
, kama vile {{ "django"|capfirst }}
, litakupa Django
.
Kama unataka kukata maandishi baada ya idadi fulani ya herufi, tumia truncatechars
. Kwa mfano, {{ "habari"|truncatechars:3 }}
litatoa Hab...
. Pia unaweza kupata urefu wa string ukitumia filter ya length
, mfano {{ "django"|length }}
litatoa matokeo 6
.
Filters hizi husaidia sana katika kuwasilisha data kwa namna iliyo rafiki kwa mtumiaji bila kuandika logic kwenye backend.
<p>Jina: {{ jina|title }}</p>
<p>Ujumbe: {{ ujumbe|truncatechars:20 }}</p>
Katika Django templates, kuna filters zinazohusika na manipulation ya namba ambazo ni muhimu kwa kuonyesha data za kihesabu kwa njia iliyoeleweka zaidi. Filter ya add
hutumika kuongeza thamani kwenye namba. Kwa mfano, {{ 10|add:"5" }}
hutoa matokeo 15
, ambapo namba 10 imeongezewa 5 moja kwa moja ndani ya template.
Filter nyingine muhimu ni floatformat
, inayotumika kuonyesha namba kwa decimal maalum. Kwa mfano, {{ 3.14159|floatformat:2 }}
i">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunz ajinsi ya kusoma mafaili na mitindo mbalimbali ya kusoma data
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza aina mbalimbali za function ambazo tunaweza kuzitumia kwenye python.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website ya Django. Hapa tutakwenda kutuma plaform ya pythonanywhere.com.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz akuhusu nadharia ya data abstraction na kazi zake kwenye OOP
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza syntaxy za python yaani sheria na kanuni za kuandika code za python
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza kwa urefu zaidi kuhusu parameter ambazo hutumika kwenye functions
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza zaidi kuhusu Jinsi ya Kuongeza Kurasa Nyingine Katika Django View
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable
Soma Zaidi...Katika somo ili utajifunza hatuwa kwa hatuwa za ku install Django, kutengeneza project na kutengeneza app
Soma Zaidi...