Katika somo hili utajifunza maana ya class, sheria za uandishi wake na mifano halisi
Class ni mojawapo ya nguzo muhimu za Object-Oriented Programming (OOP). Inarejelea blueprint au prototype inayotumika kuunda objects. Class ni aina ya mantiki ambayo inabeba attributes (tabia au mali) na methods (mbinu au kazi) ambazo zinaweza kufanywa na objects zinazotokana na hiyo class.
Fikiria mfano wa kufuatilia mbwa mbalimbali ambao wanaweza kuwa na attributes kama breed (aina) na age (umri). Ikiwa tutatumia orodha (list), inaweza kuwa vigumu kuunganisha sifa hizi kwa mpangilio mzuri, hasa tunapokuwa na mbwa wengi. Class hutatua tatizo hili kwa kupangilia data kwa njia inayoweza kudhibitiwa.
Classes zinaundwa kwa kutumia neno kuu la Python: class.
Attributes ni aina ya variables zinazohusiana na class.
Attributes zinaweza kufikiwa kupitia dot operator (.), kwa mfano: MyClass.MyAttribute.
Muundo wa class huandikwa kama ifuatavyo:
class ClassName:
# Statements au methods hapa
pass
class Dog:
pass
Attributes ni zile sifa ama properties ambazo class itakuwa nazo. Kwa mfano tukisema mbwa ndio class hivyo mbwa atakuwa na sifa kama umri, aina yake.
Tunatumia __init__() hii ni constructor ambayo inatumika kuweka attributes kwenye class. Hivyo tunaweza kuweka attribute hivi __init__(self, breed, age) baada ya hapo tutakwenda kuweka hizo attribute mfano tutaandika hivi self.breed = breed hapa tumetumia keyword self kuashiria class dog.
class Dog:
def __init__(self, breed, age):
self.breed = breed # Attribute ya aina ya mbwa
self.age = age # Attribute ya umri wa mbwa
Kwa nini tumetumia keyword self
Keyword self hutumika kuelezea class iliyopo yaani current class. Hapo ina maanisha self.age kuwa self inawakilisha class ya dog. Hata hivyo ijapokuwa keyword self ndio hutumika zaidi unaweza kuweka keyword yeyote unayoitwaka kama mbadala wa self.
Jinsi ya kuandika method kwneye class
Method huandikwa sawa na function kwani method ni function ambayo inahusishwa na class. Ndani ya class function haziitwi function bali huitwa method.
Mfano
Tuna class inayoitwa student hii itausu taarifa za mwanafunzi. Taarifa hizo ni attributes ambazo ni jina na umri.
class Student:
def __init__(self, name, age):
self.name = name
self.age = age
Sasa tunataka kuweka method inayoitwa introduce ambayo itahusika na mwanafunzi kujitambulisha jina lake na umri. Katika kutengeneza hiyo method kitu kicha kuzingatia ni kuihusisha na hiyo class. Hapa tutatumia keyword self kama ambavyo imeelezewa huko awali.
Mfano:
class Student:
def __init__(self, name, age):
self.name = name
self.age = age
def introduce(self):
return f"My name is {self.name}, and I am {self.age} years old."
Katika mfano huo class ni student, attributes ni name na age, method ni introduce. Kitu kilichobaki hapo ni kutengeneza object.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza object.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowKatika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu number method yaani function zinazofanya kazi kwenye namba.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data.
Soma Zaidi...