Katika somo hili utakwenda kujifunza zaidi kuhusu Jinsi ya Kuongeza Kurasa Nyingine Katika Django View
Baada ya kusanidi landing page katika Django kama tulivyojifunza kwenye somo lililopita, hatua inayofuata ni kuongeza kurasa nyingine kwenye mfumo wa tovuti, kama vile kurasa za nyumbani (home), wasiliana nasi (contact), blogu, na nyinginezo. Django hurahisisha sana zoezi hili kupitia mfumo wa views na URL patterns.
Katika somo hili, tutapanua app ya menu
ndani ya mradi wa PyBongo kwa kuongeza views mpya kadhaa, kila moja ikiwa na maudhui yake, na tutaunganisha kila view na URL yake husika ili mtumiaji aweze kuifikia kwa urahisi kupitia kivinjari.
Hakikisha una yafuatayo tayari:
Django tayari imewekwa kwenye mazingira yako.
Mradi unaoitwa PyBongo
uko tayari.
Ndani ya mradi, kuna app iitwayo menu
.
Fungua faili menu/views.py
kisha ongeza au hakikisha maudhui yafuatayo yapo:
from django.http import HttpResponse
def index(request):
return HttpResponse("<h1>Welcome Bongoclass.<h1>")
def home(request):
return HttpResponse("<p>This is the home page</p>")
def contact(request):
return HttpResponse("Phone number <b style='color:blue'>07653344</b>.")
def blog(request):
return HttpResponse("<u>bongoclass.com</u>")
Kila function hapo juu ni view ya Django inayoshughulikia aina fulani ya ukurasa. Zote zinatumia
HttpResponse
kuwasilisha maudhui ya moja kwa moja kwa kivinjari.
Fungua au hariri faili menu/urls.py
na hakikisha kila view imepewa URL yake kama ifuatavyo:
from django.urls import path
from . import views
urlpatterns = [
path('', views.index, name='index'),
path('home/', views.home, name='home'),
path('contact/', views.contact, name='contact'),
path('blog/', views.blog, name='blog'),
]
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhsu Template Tag nini na kazi zake. Pia utajifunza sheria za uandishi wake.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kupokea na kuchakata fomu
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz amaana ya inheritance na sheria za kuiandika inheritance.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo ili utajifunza hatuwa kwa hatuwa za ku install Django, kutengeneza project na kutengeneza app
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza Jinsi ya Kuunda Simple Navigation Menu Katika Django kwa kutumia template
Soma Zaidi...Katika somo hili uatajifunza jinsi gani unaweza kutumia view kma logic kuuma data kwenye template
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Hapa utajifunza maana ya library, kazi zake aina zake na jinsi ya ku install lirary
Soma Zaidi...