Katika somo hili utakwend akujifunz anamna ya kuwez akupata taarifa zinazohusu faili
Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kupata taarifa muhimu kuhusu faili kwa kutumia Python. Tutatumia modules zinazohusiana na os na os.path kwa taarifa za ukubwa, location, na pia tutaongeza ujuzi wa kusoma idadi ya mistari kwa kutumia mbinu tofauti.
Hakikisha faili lako lipo, na unajua jina na path yake.
Tunaweza kutumia Python standard library kufanya kazi hizi bila haja ya programu za ziada.
Ili kujua ukubwa wa faili katika bytes, tunatumia method ya os.path.getsize().
import os
# Jina la faili
file_path = 'wanafunzi.csv'
# Pata ukubwa wa faili
file_size = os.path.getsize(file_path)
print(f"Ukubwa wa faili ni: {file_size} bytes")
Output (mfano):
Ukubwa wa faili ni: 68 bytes
Ili kupata absolute path ya faili, tumia os.path.abspath().
import os
# Jina la faili
file_path = 'wanafunzi.csv'
# Pata ukubwa wa faili
file_location = os.path.abspath(file_path)
print(f"Faili lipo katika: {file_location}")
Output (mfano):
Faili lipo katika: /home/user/projects/wanafunzi.csv
Tumia os.path.getmtime() kupata muda wa mwisho faili liliposasishwa (editing). Taarifa hii itarudiwa kama timestamp ya UNIX ambayo inaweza kubadilishwa kuwa fomati inayosomeka.
import os
import time
# Jina la faili
file_path = 'wanafunzi.csv'
# Muda wa mwisho wa kusasisha
last_modified = os.path.getmtime(file_path)
print(f"Faili lilisasishwa mwisho: {time.ctime(last_modified)}")
Output (mfano):
Faili lilisasishwa mwisho: Tue Dec 3 12:45:00 2024
Tumia os.path.getatime() kupata muda wa mwisho faili lilipotumika.
import os
import time
# Jina la faili
file_path = 'wanafunzi.csv'
last_accessed = os.path.getatime(file_path)
print(f"Mara ya mwisho faili lilipotumika: {time.ctime(last_accessed)}")
Output (mfano):
Mara ya mwisho faili lilipotumika: Tue Dec 3 13:00:00 2024...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza jinsi Django hutumia migrations kuunda na kubadilisha tables kwenye database kulingana na models tunazoandika. Tutapitia maana ya migration, hatua za kuitumia, umuhimu wake, misingi ya makemigrations na migrate, pamoja na mfano halisi kutoka kwenye project yetu ya pybongo (app: menu).
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kutumia Django ORM kufanya mahesabu mbalimbali kama Sum, Avg, Count, Max, Min, pamoja na kupunguza idadi ya items zinazoonekana kwenye dashboard (LIMIT). Pia tutajifunza namna ya kutengeneza βdifferenceβ kati ya thamani kubwa na ndogo bila kubadilisha functions zozote ulizokwisha ziandika.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya class, sheria za uandishi wake na mifano halisi
Soma Zaidi...Somo hili linazungumzia hatua ya kuunda navigation menu na kutumia template inheritance kwa njia ya kitaalamu katika Django.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutajifunza jinsi ya kuunda dashboard rahisi ndani ya Django ambayo itaruhusu mtumiaji kuongeza, kusoma, kuhariri na kufuta taarifa za MenuItem bila kutumia Django built-in admin, bali kwa kutumia HTML templates na views tulizotengeneza sisi wenyewe.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza kwa urefu zaidi kuhusu parameter ambazo hutumika kwenye functions
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu string indexing. Kama tulivyojifunza kuhusu namba katika somo lililopita, basi hapa tutakwenda kucheza na string.
Soma Zaidi...