Katika somo hili tunakwenda kujifunza matumizi ya break na continue kwenye loop
Katika somo hili, tutajifunza jinsi ya kutumia break na continue kwenye loop za Python. break na continue hutumika kudhibiti mtiririko wa utekelezaji wa loop:
break hutumika kukatisha utekelezaji wa loop kabisa.
continue hutumika kuruka hatua fulani ya loop na kuendelea na hatua inayofuata.
Break hutumika pale unapotaka kusitisha utekelezaji wa loop mara moja baada ya kufikiwa kwa sharti fulani.
Hapa, tutasimamisha utekelezaji wa loop mara tu tunapofika namba 8.
print("TEBO YA 7:")
for x in range(1, 13): # Kuanzia 1 hadi 12
if x == 8:
break
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Matokeo: Loop itazalisha hadi 7 * 7 = 49 kisha kusimama.
Continue hutumika kuruka hatua fulani kwenye loop bila kusitisha loop nzima.
Hapa, tutaruka namba 8 na kuendelea na 9.
print("TEBO YA 7 (TUNARUKA 8):")
for x in range(1, 13):
if x == 8:
continue
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Matokeo: 7 * 8 = 56 haitajumuishwa kwenye matokeo.
Hapa, tutaruka namba zote kati ya 5 na 8.
print("TEBO YA 7 (TUNARUKA 5 HADI 8):")
for x in range(1, 13):
if 5 <= x <= 8:
continue
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Hapa, tutasimamisha utekelezaji wa loop mara tu tunapofika namba 8.
print("TEBO YA 7 (BREAK):")
x = 1
while x <= 12:
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
if x == 8:
break
x += 1
Hapa, tutaruka namba 8 kwenye utekelezaji wa loop.
print("TEBO YA 7 (CONTINUE):")
x = 0
while x < 12:
x += 1
if x == 8:
continue
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Python haina do while loop asili, lakini tunaweza kuunda dhana hiyo kwa kutumia while na break.
Hapa, loop itatekelezwa mara moja hata kama sharti halijafikiwa, kisha itasitisha mara baada ya kufika namba 8.
print("TEBO YA 7 (DO-WHILE NA BREAK):")
x = 1
while True:
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
if x == 8:
break
x += 1
Hapa, tutaruka namba 8 na kuendelea na 9.
print("TEBO YA 7 (DO-WHILE NA CONTINUE):")
x = 0
while True:
x += 1
if x == 8:
print("Namba 8 haipo")
continue
if x > 12:
break
print(f"{x} * 7 = {x * 7}")
Katika somo hili, umejifunza:
Jinsi ya kutumia break kukatisha utekelezaji wa loop.
Jinsi ya kutumia continue kuruka hatua fulani kwenye loop.
Somo linalofuata: Jinsi ya kupata user input kwenye programu zako. Endelea kufanya mazoezi!
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Hapa tunakwenda kujifunza kuhusu OOP ambapo ni miongoni mwa mitindo ya uandishi wa code
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kuandika function, kuweka parameter na kuitumia function
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza operator nyingine kama assignment operator logical, identity operator na membership operator.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz ajinsi ya kutumia html kwneye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya class, sheria za uandishi wake na mifano halisi
Soma Zaidi...