Hapa utakwenda kujifunz amaana ya package, aina zake na jinsi ya kuandika package.
Package kwenye Python ni mkusanyiko wa modules zilizoandaliwa ndani ya folda moja. Package hutumika kupanga modules zinazohusiana pamoja ili kurahisisha upatikanaji, urejelevu wa msimbo, na usimamizi wa miradi mikubwa ya programu.
Kwa nini kutumia Package?
Kusaidia kupanga msimbo wa programu kwenye miradi mikubwa.
Kuruhusu kushirikisha msimbo baina ya modules kwa urahisi.
Kupunguza mgongano wa majina ya modules kwa kutumia namespace.
Tofauti kati ya Module na Package:
Module ni faili moja la .py.
Package ni folda yenye modules moja au zaidi.
Package inawakilishwa na folda yenye faili moja maalum linaloitwa __init__.py.
__init__.py linaweza kuwa tupu au kuwa na msimbo unaohitajika kuanzisha package.
Python inatambua folda yenye faili la __init__.py kama package.
Tengeneza package inayoitwa hesabu yenye modules mbili: eneo.py na volum.py. Zingatia kuwa ili folda liite package lazima kuwepo na faili linaloitwa _ _init_ _.py
Muundo wa Folda:
hesabu/
│
├── __init__.py
├── eneo.py
└── volum.py
eneo.py:
def mraba(urefu, upana):
return urefu * upana
def pembetatu(kimo, kitako):
return (kimo * kitako) / 2.0
volum.py:
def mchemraba(urefu):
return urefu ** 3
def silinda(r, h):
return 3.14159 * (r ** 2) * h
__init__.py:
Hili faili linaweza kuwa tupu au kuorodhesha modules zinazopatikana kwenye package. Kwa mfano:
from .eneo import mraba, pembetatu
from .volum import mchemraba, silinda
Tumia package yako kwenye programu: main.py
from hesabu.eneo import mraba, pembetatu
from hesabu.volum import mchemraba, silinda
print(f"Eneo la mraba: {mraba(4, 5)}") # 20
print(f"Eneo la pembetatu: {pembetatu(4, 6)}") # 12.0
print(f"Volum ya mchemraba: {mchemraba(3)}") # 27
print(f"Volum ya silinda: {silinda(2, 5)}") # 62.8318
Unda folda na upe jina lako. Hii ndio itakuwa package yako, kwa mfano mahesabu.
Faili hili linahitajika ili Python itambue folda kama package. Linaweza kuwa tupu au lisiwe tupu kulingana na mahitaji yako.
Andika modules tofauti kwa kazi maalum ndani ya package yako.
Tumia import kuleta package au modules kutoka kwenye package yako.
Package inaweza pia kuwa na sub-packages, ambazo ni packages ndogo ndani ya package kubwa.
project/
│
├── hesabu/
│ ├── __init__.py
│ ├── eneo/
│ │ ├── __init__.py
│ │ ├── mraba.py
│ │ └── pembetatu.py
│ └── volum/
│ ├── __init__.py
│ ├── silinda.py
│ └── mchemraba.py
└── main.py
hesabu/eneo/mraba.py:
def eneo(urefu, upana):
return urefu * upana
hesabu/eneo/pembetatu.py:
def eneo(kimo, kitako):
return (kimo * kitako) / 2.0
hesabu/volum/silinda.py:
def volum(r, h):
return 3.14159 * (r ** 2) * h
hesabu/volum/mchemraba.py:
def volum(urefu):
return urefu ** 3
hesabu/__init__.py:
from .eneo import mraba, pembetatu
from .volum import silinda, mchemraba
Kwenye main.py:
from hesabu.eneo.mraba import eneo as eneo_mraba
from hesabu.volum.silinda import volum as volum_silinda
print(f"Eneo la mraba: {eneo_mraba(5, 4)}") # 20
print(f"Volum ya silinda: {volum_silinda(3, 7)}") # 197.92034
Kuweka msimbo ulioandaliwa vizuri: Inarahisisha kusimamia miradi mikubwa.
Kuongeza urejelevu: Modules zilizopo kwenye package zinaweza kutumika tena.
Namespace: Huzuia migongano ya majina ya functions au variables.
Packages ni njia ya juu ya kupanga msimbo wako wa Python. Kwa kutumia folda, __init__.py, na modules, unaweza kuunda miradi inayoweza kudhibitiwa kwa urahisi na kutumia tena msimbo mara nyingi. Packages husaidia programu kuwa safi, rahisi kudhibiti, na kubadilika kwa mahitaji makubwa ya miradi ya kisasa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tunakwenda kujifunza aina nyingine za data ambazo hutumika kwenye python.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jisni ya kujuwa aina ya data iliyotumika kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz ajinsi ya kutengeneza folda, faili na kuweka data kwneye faili
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu maana ya python na kazi zake. pia jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku host website ya Django. Hapa tutakwenda kutuma plaform ya pythonanywhere.com.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz akutumia database kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili uatajifunza jinsi gani unaweza kutumia view kma logic kuuma data kwenye template
Soma Zaidi...Katika soo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubaduli aina moja ya data kwena aina nyingine. Kwa mfano unaweza kubadili namba kuwa string ama kubadili string kuwa nanda ama kubadili float kuwa int.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujfunza operator nyingine kama assignment operator logical, identity operator na membership operator.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya django framework na inafanya kazi gani
Soma Zaidi...