Katika somo hili utajifunza maana ya encapsulation na sheria za uandishi wake
Encapsulation ni dhana ya kuficha data ya ndani ya object ili isiweze kufikiwa moja kwa moja kutoka nje ya class.
Hii inamaanisha kuwa property au method iliyo ndani ya class haiwezi kufikiwa au kubadilishwa moja kwa moja kutoka nje.
Kwa kutumia encapsulation, tunaweza kudhibiti jinsi data inavyopatikana au kubadilishwa kupitia mbinu (methods) maalum.
Lengo kuu ni:
Kulinda data dhidi ya mabadiliko yasiyotarajiwa.
Kuweka mipaka ya ufikiaji ili kuboresha usalama wa programu.
Ulinzi wa Data: Inawezesha kudhibiti jinsi property na method za object zinavyofikiwa au kubadilishwa.
Kupunguza Makosa: Inazuia mabadiliko yasiyoidhinishwa kwenye data.
Rahisi Kudhibiti: Programu inakuwa rahisi kuelewa, kudumisha, na kufanya marekebisho bila kuvunja sehemu nyingine.
Usalama: Huzuia ufikiaji wa moja kwa moja wa data muhimu kutoka nje ya class.
Ili kufanikisha encapsulation, tunatumia viwango vya ufikiaji vya property na method kwenye class. Python hutoa viwango vitatu vya msingi:
Property na method zinazoonekana na kufikiwa moja kwa moja kutoka nje ya class.
Kwa kawaida attribute zinakuwa ni public by default.
Mfano:
class Example:
def __init__(self):
self.data = "Public Data" # Public
obj = Example()
print(obj.data) # Inaweza kufikiwa moja kwa moja
Property na method zinazofikiwa ndani ya class husika na class zilizorithi (subclasses). Kuhusu class zinazorithi tutajifunza mbeleni.
Hutangulizwa na alama ya underscore moja _.
class Example:
def __init__(self):
self.data = "Protected Data" # Private attribute
# Kufikia private attribute moja kwa moja nje ya class
obj = Example()
print(obj.data)
Katika mfano huo tumeweza kuprint attribute data bila ya tatizo nje ya class. Huu ni mfano wa public. Lakini sasa hebu tufanye attribute data kuwa protected.
Mfano
class Example:
def __init__(self):
self._data = "Protected Data" # Private attribute
# Kufikia private attribute moja kwa moja nje ya class
obj = Example()
print(obj._data)
Pia kuna namna ambavyo protected inaweza kutumika lakini sio njia inayoshauriwa kutumia yaani haipendezi.
Mfano:class Example:
def __init__(self):
self._data = "Protected Data" # Protected
obj = Example()
print(obj._data) # Inaweza kufikiwa lakini haipendekezwi
Mfano wa kurithi protected
class Parent:
def __init__(self):
self._data = "Protected Data" # Protected attribute
def display_data(self):
print(f"Data from Parent: {self._data}")
class Child(Parent):
def modify_data(self, new_data):
self._data = new_data # Accessing and modifying protected attribute
print(f"Data modified in Child: {self._data}")
# Kutengeneza object ya Child class
child_obj = Child()
# Kufikia na kuonyesha protected attribute kupitia parent method
child_obj.display_data() # Output: Data from Parent: Protected Data
# Kufikia na kubadilisha protected attribute kupitia child method
child_obj.modify_data("New Protected Data") # Output: Data modified in Child: New Protected Data
# Kuhakikisha mabadiliko yanadumu
child_obj.display_data() # Output: Data from Parent: New Protected Data">...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utajifunz akutumia database kwenye python
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunz anamna ya kuwez akupata taarifa zinazohusu faili
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza aina za data ambazo hutumika kwenye python. hapa utajifunza aina kuu 3 za data.
Soma Zaidi...Ni nini maana ya django framework na inafanya kazi gani
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya polymorphism na sheria za uandishi wake
Soma Zaidi...Katika somo hili uatkwenda kujifunz anamna ambavyo mtu anaweza kuingiza input kwneye system
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili ukurasa wa landing page wa Django na kuweka ukurasa tunaoutaka sisi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza maana ya object, na sheria za kuandika object.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza maana ya variable, na sheria za kutengeneza variable kwenye python. Pia utajifunza maneno ambayo hayafai kutumiwa kama variable
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia while loop kwneye python
Soma Zaidi...