PHP - somo la 30: Baadhi function za PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ktumia baadhi ya function za php
BUILT IN FUNCTIONS
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu functions ambazo zimetengenezwa moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji wa PHP. Hapa nitakuchagulia baadhi tu ya function ambazo hatukuziona kwenye level 1. Hivyo kama utahitaji kujuwa functions zaidi rudi kwenye PHP level 1.
pi()
Function hii hutumika kwa ajili ya kupata tyhamani ya pi (pai) kwa wale wa hesabu wanaelewa pi ni nini kwenye kutafuta eneo la duara, nusu duara n.k
Mfano 1:
<?php
echo(pi());
?>
min() na max()
Hizi kwa pamoja hutumika kutafuta namba kubwa na ndogo. max() ni kwa ajili ya kutafuta nmab kubwa kwenye orodha ya namba. Na min() kazi yake ni kutafuta namba ndogo kwenye orodha ya namba.
Mfano2:
<?php
echo(min(16, 450, 70, 20, 18, 35) . "<br>");
echo(max(67, 210, 51, 20, -16, -12));
?>
sqrt()
Function hii hutumika katika kutafuta square root ya namba. Wale wa hesabau wanafaham vyema hii function.
Mfano 4
<?php
echo(sqrt(9) . "<br>");
echo(sqrt(50) . "<br>");
echo(sqrt(16) . "<br>");
echo(sqrt(81));
?>
5. rand()
Function hii hutumika kwa ajili ya kutengeneza random namba. Hii inaweza kutumika kama kutengeneza unique id. Japo tutaona function nyinginezo zitakazotumika sawa na hii.
Mfano 5:
<?php
echo(rand());
?>
Sasa endapo kwa mfano unahitaji random namba hizi zitokee katika mpangilio fulani. Kwa mfano unataka random namba ziwe kati ya 18 na 67. Yaani namba ndogo iwe ni 18 na namba kubwa iwe ni 67. Hivyo random namba zicheze humo. Kufanya hivi itakubiidi utumie parameter ndani ya functuin. Kwa mfano kwenye maelezo hayo itakuwa hivi:
Mfano 6:
<?php
echo(rand(18, 67));
?>
6. uniqid()
Function hii hutumika kuzalisha namba ambazo ni unique yaani haziwezi kufanana. Hii ni muhimu katika ktengeneza id za item kwenye database.
Mfano 6:
<?php
echo uniqid();
?>
7. session_start()
Function hii hutumika kwa ajili ya kuanzisha session ama kupata taarifa...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
PHP somo la 53: class inheritance kwenye PHP Object Oriented Programming
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class inheritance kwenye object oriented programming.
Soma Zaidi...PHP somo la 66: Jinsi ya ku edit data na kufuta kwenye database kwa kutumia PDO
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi jinsi ya ku edit ama ku update data na kuzifuta kwenye database kwa kutumia PDO
Soma Zaidi...PHP - somo la 10: Jinsi ya kundika condition statement if, ifelse na switch case
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu condition statements if, ifelse na switch case. Hata utajifunza jnsi ya kuziandika na zinavyofanya kazi
Soma Zaidi...PHP - somo la 14: Jinsi ya kutengeneza database kwa kutumia PHP
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia PHP kutengeneza database kwenye mysql database.
Soma Zaidi...PHP somo la 98: Library za PHP ambazo unaweza kutumia ORM
Somo hili litakwenda kukutajia baadhi ya library za php ambazo hutumika kwa matumizi ya ORM
Soma Zaidi...PHP - somo la 32: Jinsi ya kutumia filter_var() function kwenye PHP
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia filter_var() function kwa ajili ya kuchuja code zilizo hatari kwenye PHP file
Soma Zaidi...