Maana ya afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya afya
MAANA YA AFYA
Afya ni hali ya kuwa mzima kimwili na kiakili. Kuna mahusiano makubwa kati ya kuwa mzima kimwili na akili. Mtu anaweza kuwa mwili upo mzima kabisa lakini akaambiwa hana afya salama kwa maana anaweza kuwa akili yake haipo vizuri. Kuathirika kiakili pia ni ugonjwa na ndio maana kuna wagonjwa wa sikolojia.
Hivyo mtu mwenye afyqa ni yule a,baye ni mzima wa mwili na akili. Na tunaposema akili haimaanishwi mgonjwa wa akili ni yule mkichaa hapa na bali hata ambaye saikolojia yake haipo vizuri nae ni mgonjwa.
Ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo ambayo hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa mwili haudhuriki kimwili na kiakili. Mifumo hii ipo kazini muda wowotw kupambana na mamilioni ya wadudu hatari waliopo kwenye mazingira yetu. Kwa mfano kwenye hewa kuna mabilioni ya wadudu kama bakteria ambao huambukiza maradhi.
Mwili unaweza kuthibiti maradhi kupitia njia zake nyingi kwa mfano;- katika mfumo wa damu kuna seli hai nyeupe za damu hizi zinapambana na vijidudu vya maradhi. Halikadhalika mna katika damu antibodies hizi zinafanya kazi hii pia. Kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuna asidi ambazo zinakazi ya kuuwa bakteria na vijidudu vingine vya maradhi. Kwenye mfumo wa upumuaji kuna uttelezi na vijinywele ambavyo hukamata vijidudu pamoja na mavumbi na kutolewa nje.
Hivyo mwili una mfumo madhubuti kabisa wa kuweza kupambana na maradhi. Na ikitokea umepambana na kushindwa hapo hutokea mtu akaumwa. Pia ijulikane kuwa kinga za mwili zinaweza kutengenezwa na mwili wenyewe au kuzipata kwa kutumia chanjo. Mwili huanza kutengeneza kinga hizi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto na hivyo hivyo mwili huendelea kuzitengeneza kinga hizi wakati wa kukua na kuendelea kwa maisha baada ya kuzaliwa.
Pia wakati mwingine mapambano yanapokuwa makali ndani ya mwili huweza kutokea maumivu katika sehemu za mwili. Kwamfano mfumo wa lymph unapopambana vikali huweza kusababisha maumivu ya mtoki
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Madhara ya kuchelewa kutibu tatizo la kiafya
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea endapo tatizo halijatibiwa.
Soma Zaidi...Utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyeaha
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo.
Soma Zaidi...Mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...Namna ya kujikinga na kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia au kujikinga na kifua kikuu, hizi ni njia ambazo utumika ili kujikinga na kifua kikuu
Soma Zaidi...Aliyepaliwa na maji huduma ya kwanza itakuwaje
Vipi utamsaidia mti ambaye amepaliwa na maji? Post hii itakwenda kukifundisha jambo hili.
Soma Zaidi...