Menu



Yanayoathiri afya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayoathiri afya

YANAYOATHIRI AFYA

Afya yamtu inaweza kuathiriwa kuwa njema au kuwa mbovu kwa kuzingatia mambo kadhaa wakadhaa. Hapa nimechagua mambo makuu matano ambayo nitakwenda kuyaangalia ambayo ni;-

 

A).vyakula

B)Mazingira

C)Shughuli za kila siku

D)Tabia na mazoea

E)Vizazi, familia ama kurithi.

 

1.VYAKULA

Vyakula ni katika sababu kubwa ambazo husaidia kwa kiwango kikubwa kuathiri afya za watu. Wataalamu wa afya leo wanaeleza na kutaja magonjwa mengi sana ambayoyo yanapatikana kwa kupitia vyakula. Pia yapo magonjwa ambayo huambukizwa kwa kupitia ulaji wa chakula. Hivyo magonjwa mengi na hatari zaidi yamekuwa na mahusiano na vyakula vyetu. Chakula kinaweza kuwa msaada kwako au kuwa ni chanzo cha matatizo ya afya yako. Mfano mzuri ni kuwa leo wataalamu wa afya anaeleza kuwa mamilioni ya watu wanakufa kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa miongoni mwa sababu za ugonjwa huu ni vyakula. Vyakula ambavyo tunavila leo sio rafiki kwa afya zetu. Tumekuwa tukila vyakula ambavyo vimejaa kemikali nyingi na matatizo kadha wakadha.

 

Mfano wa pili ni ugonjwa wa kisukari, huu ugonjwa umekuwa ukienea kwa kasi sana duniani leo. Kuanzia watoto, vijana wazee na wajawazito wote wapo hatarini kuapata maradhi haya. Wataalamu wa afya wanataja kuwa vyakula ni katika sababu mjawapo ya kupata maradhi haya. Kuongezeka kwa uzito nje ya uzito wa kawaidi ni katika sababu za kutokea kwa kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula ni sababu ya kuongezeka kwa uzito mwilini na kutofanya mazoezi ijapokuwa zipo sababu zingine.

 

Magonjwa ya moyokama shinikizo la damu (presha) pamoja na shambulio la moyo (heart attack) ni katika magonjwa yanayowapata watu weng duniani na kusababisha vifo vingi sana. Wataalamu wa afya wanaeleza katika sababu kubwa za kutokea kwa maradhi haya ni vyakula. Hususan vyakula vyenye mchanganyiko mkubwa wa mafuta ya viwandani.

 

Maradhi ya utapiamlo kama matege, baadhi ya matatizo ya macho, unyafuzi na kwashiakoo pamoja na kudumaa ni katika maradhi ambayo husababishwa na vyakula. Majeraha kutokupona haraka, kuchelewa kupona kwa vidonda na makovu, ngozi kupasuka na kutokwa na vidonda kwenye mdomo ni katika baadhi ya matatizo yanayosababishwa na vyakula Kwa ufupi ni kuwa vyakula ni katika sababu kubwa sana ya maradhia mabayo tuanayapata. Tutazungumzia kwa undani zaidi somo hili kwenye kurasa zijazo na tutaona kwa undani vipi vyakula vinaweza kusababisha yote hayo.

 

2.MAZINGIA

Mazingira yamekuwa leo ni sababu ya kupata maradhi mengi sana. Maradhi mengi yanayotupata kutokana na mazingira yetu yanaweza kusababishwa na uchafu wa mazingira. Ijapokuwa mazingira yanaweza kuwa safi na pia yakasababisha maradhi. Mazingira pia yanaweza kuwa msaada kwetu kwa kuweza kulinda na kuimarisha afya zetu. Ila kwa ufupi hapa tutazungumzia tuu mazingira yanavyoathizi afya zetu kuwa dhoofu.

 

Mfano mzuri ni maradhi ya malaria ambayo leo yamekuwa yakipelekea mamilioni ya vifo duniani hususani watoto waliopo chini ya umri wa miaka mitano. Malaria yanaenezwa na mbu aina ya anofelesi na mbu huyu ni jike. Mbu hawa wanazaliana sehemu zenye majimaji. Mbu hawa hawahitaji maji mengi sana, hapana hata tone moja linamtosha yeye kutaga na kutoa watoto. Mbu hawa wamekuwa wakipatikana kwenye mazingira yetu. Wataalamu wa afya wanaeleza usafi wa mazingira kama kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ni katika njia za kupambana na maradhi haya.

 

Mfano mwingine ni m aradhi ya kipindupindu, haya yamekuwa yakisababishwa na bakteria ambao wanaingia mwilini kwa njia ya chakula. Mazingira yanaweza kuwa njia ya kuenezxa maradhi haya kama usafi wa mazingira hautazingatiwa. Nzi wanaweza kubeba vijidudu vya maradhi na kuvipeleka kwingine katika mazingira yasiyokuwa safi.

 

Maradhi ya mafua yamekuwa ji kawaida sana kwa nchi zilizopo kwenye tropic. Maradhi yaya yanaweza kupatikana sana kwenye mazingira yenye vumbi sana. Pia kupitia hewa kutoka mgonjwa kwenda mtu mzima. Hivyo tunaweza sema mafua yanaenezwa sana kwenye mazingira kupitia hewa.

 

--> Wataalamu wa afya wanaeleza maradhi mengi sana ambayo hupatikana kwenye mazingira yetu yakila siku. Mazingira haya yanaweza kuwa kwenye maji kama maradh ya kichocho, kwenye hewa kama kifua kikuu na mafua au mazingira ya chini kama vile maradhi ya kipindupindu.

 

3.SHUGHULI ZA KILA SIKU

HAlikadhalika shughuli zetu za kila siku zinaweza kuwa sababu mojawapo ya kupata maradhi mablimbali za kutafutia riziki zinaweza kuwa sababu tosha ya kupata maradhi. Wataalamu wanaeleza maradhi kazaa ambayo yanaweza kuwa chanzo chake ni shughuli zetu za kila siku.

 

Vifaa vya kufanyia kazi kama visipotumika ipasavyo kwa mfano kuvaa viatu maalumu na nguo maalumi kwa ambao wanafanya kazi viwanda vya kemikali, wanaweza kupata madhara. Wafanyaji kazi sehemu zenye mionzi hatari kama x-ray wasipovaa mavazi maalumu kwa utaratibu husikwa wanaweza kuapata madhara.

 

Muda wa kufanya kazi usipizingatiwa pia madhara yanaweza kuapatikana. Kwa mfano sehemu zenye mionzi mikali kama x-ray kuna muda maalumu wa kufanya kazi na ukipita anatakiwa aingie mtu mpya. Hivyo jkazi kama hizi muda usipizingatiwa madhara ya kiafya yanaweza kutokea.

 

Halikadhalika teknolojia inayotumika kufanyika kazi kama haitakuwa katika hali nzuri inaweza kusababisha madhara. Vifaa vya kisasa vinatakiwa vitumike zaidi kwa ajili ya usalama kuliko kuendelea na vile vya zamani vinavyohitaji nguvu nyingi na kufanya kazi mazingira ya hatari.

 

Hivyo shughuli zetu za kufanyia kazi zsipowekwa katika hali nzuri zinaweza kuwa ni sababu ya sisi kuapata madhara makubwa kama kupiteza mali, kupoteza uhai au kupoteza viungo vya miili yetu. Somo hili tutaliona kwa undani zaidi kwnye kurasa zijazo.

 

4.TABIA

Tabia za watu pia zinaeza kuwa ni sababu ya kupata maradhi na kuathiri afya. Watu wamekuwa wakikulia katika koo, familia na kabila mbalibali ambapo wanajifunza tabia tofautitofauti. Tabia hizi kama hazitakuwa katika hali inayotakiwa zinaweaa kusababisga kupata maradhi

 

Nitoe mfano mzuri kuhusu maradhi ya fangasi sehemu za siri. Fangasi hawa wanafurahia sana mazigira yenye majimaji. Mara nyingi usafi wa nguo za ndani na mwili kwa ujumla hususan sehemu zile umaweza kuwa sababu ya kuendelea kuwalea wadudu hawa. Tabia ya kuvaa nguo mbichi hususani zile za ndni inaweza kuendelea kuwalea fangasi hawa.

 

Tabia ya kula mara kwa mara inaweza kusababisha kupata kitambi. Mtu akiwa anakula mara kwa mara bila ya kufanya mazoezi anaweza kupata tatizo la kuzidi kwa uzito. Tatizo hili linaweza kuathiri mwili kushindwa kuzalisha homoni za insulin kwa kiwango kinachotakiwa na hatimaye kupata kisukari.

 

Tabia ya kuchelewa kualal yaani kukosa muda mzuri wa kulala inaweza kuwa sababu ya kupata matatizo ya kiafya. Mwili unahitaji muda wa kutosha wa kulala ili uweze kurekebisha mwili ndani ya muda huo. Mwili unahitaji kupumzika pia.

 

Tabia ya kukaana misongo ya mawazo na kupenda kukasirika na kukaa na vinyongo. Hii ni hatari sana ka afya ya mtu kisaikolojia na kimwili pia. Misongo ya mawazo inaweza kuwa sababu nzuri ya kupata maradhi kama vidonda ya tumbo. Maumivu ya kichwa na tumbo pia huweza kuletwa na misongo ya mawazo

 

5.VIZAZI, FAMILIA NA KURIDHI (GENETICS)

Afya ya mtu inaweza kuathiriwa na kurithi kutoka kwa wazazi. Hapa mtu hana chaguo maana kurithi huku kumetokea toka tumboni kwa mama. Mtu anaweza kurithi maradhi kama pumu, moyo, kisukari, siko seli na mengineyo.

 

Kwa ufupi hivi vipengele vinavyoathiri afya tutaviona kwa undani zaidi kwenye kurasa zijazo. Hapo tumeona tuu juu juu namna ya mabo yalivo. Sasa hebu tuone vitu tutaweza kuboresha afya zetu.

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 1734


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Uvutaji wa sigara
Somo Hili linakwenda me kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara Soma Zaidi...

Nini husababisha kibofu cha mkojo kuuma na baadae kutoka damu
Katika post hii utajifunza sababu zinazowezabkuorlekea kibofu kuuma upande mmoja Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATA JOTO LA JUU ZAIDI (HEAT STROKE)
Hii ni hali inayotokea ambapo wili unakuwa na joto la juu sana tofauti na kawaida. Soma Zaidi...

Njia za kupunguza uzito na kitambi
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa pamoja na kitambi Soma Zaidi...

Maana ya afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya afya Soma Zaidi...

Mbinu za kuponyesha majeraha
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo hutumika kuponyesha majeraha kwa haraka zaidi,tunajua majereha utokana na kupona kwa vile vidonda au kupona kwa sehemu ambayo imekuwa na majeraha kwa hiyo ili kuponyesha majeraha hayo tunapaswa kufanya yafuatayo. Soma Zaidi...

Zijue kazi za chanjo ya DTP au DPT (Donda Koo,Pepopunda, na kifaduro))
Posti hii inahusu zaidi kazi ya chanjo ya DTP au DPT ambayo Inazuia magonjwa ya Donda Koo, Pepopunda na kifaduro. Soma Zaidi...

Umuhimu wa uterusi
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa uterusi, ni mfuko unayosaidia kumtunza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu virutubisho vya wanga na kazi zake mwilini
Katika vyakula tunaposema wanga tunamaanisha virutubisho ambavyo hupatikana kwenye vyakula. Hivi husaidia sana katika kuifanya miili yetu iwe na nguvu. Soma Zaidi...

Mambo yanayoweza kudhoofisha kinga ya mwili
Kinga ya mwili inapodhoofu mwili unakuwa hatarini kupata maradhi. Je unayajuwa mambo yanayodhoofisha kinga ysbmeili? Soma Zaidi...