image

Kuboresha afya

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayosaidia kuboresha afya

KUBORESHA AFYA

1.TAHADHARI KWENYE VYAKULA

Ukiweza kuchukuwa tahadhari kwenye vyakula na kujua chakula salama cha kukila kulingana na mahitaji ya mwili hapa unaweza kufanikiwa kuulinda mwili wako na maradhi mengi sana. Uwe na elimu sahihi ya vyakula na faida zake kwenye mwili. Kwani unaweza kukusanya vyakula vingi kumbe ni sawa na kual chakula kimoja

 

Vyakula vya protini ni m uhimu katika ukuaji wa watoto na ukuaji wa tishu. Vyakula hivi huhusika katika kuurekebisha mwili na ni muhimu hsana katika kuhakikisha afya ya mtu ipo kwenye msitari mzuri. Kwa ufupi tunasema kuwa vyakula vya protini ni vyakula vya kujenga mwili. Unaweza kupata protini kwenye maziwa, samaki, nyama, maini, maharage na mayai. Upungufu wowote wa vyakula hivi unaweza kuleta mdahara makubwa kama tulivyoona hapo juu.

 

Vyakula vya wanga ni mujarabu sana kwa ajili ya kuupa mwili nguvu. Tumia vyakula hivi hasa kama unafanya kazi za nguvu. Vyakula hivi pia ni muhimu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa m ifumo ndani ya mwili inafanya kazi kwa usahihi. Kwa mfano mfumo wa upumuaji na uunguzwaji wa chakula (espiration) unahitajia vyakula hivi kwa ajili ya kuzalisha nguvu ya kutosha ndani ya mwili. Vyakula hivi vinaweza kupatikana kwenye nafaka kama mahindi, ngano na mchele.

 

Vyakula vya madini, Mwili unahitaji vyakula hivi ili uwezesjhe matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Vitamin c hujulikana kwa kusaidia ugonjwa wa scuvy ugonjwa huu humfanya mtu atoke samu mwenue mafinzi. Vitamin A husaidia kurekebisha afya ya macho. Vitamin K husaidia kuganda kwa damu unapopata jeraha. Mwili unahitaji madini pia ili uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno. Madini na vitamin hpatikana zaidi kwenye mboga za majani, na matunda. Matunda yenye uchachu kama limao, chungwa husaidia kwa vitamin C na mapapai pi hujulukana kwa kuwa na vitamin C. spinachi ni muhimu kwa vitamin A. samaki husaidia kwa madini mengine.

 

Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu. Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku. Hivyo mtu awe na tahadhari zaidi juu ya kupangilia vyakula vyake. Tuatona zaidi aina hizi na madhara yake kwenye kurasa zijazo.

 

Unywaji wa maji ni jambo linalolazimishwa sana. Kwama mtu hana sababu yeyote anatakiwa anywe maji mengi zaidi. Wataalamu wa afya wanashauri angalau kwa siku mtu anywe maji bilauri (glass) nane kwa kiwango cha chini. Mwili wa kiumbe hai asilimia 50-90 ni maji. Hivyo maji yakipungua mwilini kunaweza kutokea madhara makubwa zaidi. Maji huhitajika karibia katika mifumo yote mwilini. Maji hutumika katika kurekebisha afya ya mtu.

 

2.TAHADHARI KWENYE MAZINGIRA

Kama tulivyoona hapo juu, mazingira yetu ni sababu tosha ya kuathiri ubora wa afya zetu. Hivyo mtu ahakikishe sikuzote anaishi katika mazingira salama na safi. Wataalamu wa afya wanatueleza kusafisha mazingira yetu ya ilasiku ili tuweze kukabilia na na wadudu hatara.

 

Hakikisha hewa unayoipata ni safi na salama. Futa mavumbi ndani ya nyumba na nguo za kujifunika ziwe safi, kwa namna hii ni rahisi kukabilia na na mafua. Epuka moshi kutoka viwandani, pia usilale ukiwa na jiko la mkaa linalowaka na ikawa madirisha na milango umefunga. Unaweza kupata tatizo la kukosa oxkyjeni na kufariki dunia. Kaa mbali na wavuta sigara kwani hewa yao inaweza kukuathiri na wewe pia. Jambo la msingi hapa ni kuchukua tahadhari dhidi ya hewa ambayo tunaipata kwenye mazingira hetu.

 

Hakikisha unafyeka na kupunguza nyasi zilizo karibu na wewe. Fukia madimbwi na majimaji yoyote yalotuwama hata kama yapo kwenye kifuniko cha soda kwani hayo ni machache lakini mamia ya mbu yanaweza kuzaliana hapo. Mashimo ya kutupia taka yawe mbali kidogo na nyumba na kuwepo utaratibu wa kuchoma moto mashimo hayo bada ya muda. Usafi wa mazingira unaweza kuwa njia tosha ya kuanza harakati za kukabiliana na malaria na kipindupindu.

 

Watu wahakikishe wanakunywa maji safi na salama pamoja na kula vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa usalama. Usafi wa maji unaweza kuwa njia ya kupambana na typhod (taifodi) na maradhi mengine ya tumbo. Kuwepo na utaratibu wa kuyatibu maji kama yamepatikana sehemu ambazo sio salama na safi. Maji yanaweza kutibiwa kwa njia za kisasa kama kuweka madawa. Lakini pia unaweza kutumia njia ya kuyachemsha na kuyachuja na kuyatumia.

 

Sikuzote hakikisha unaishi katika mazingira rafiki na afya yako. Watu ambao tayari wanamaambukizi ya maradhi maalumu wanatakiwa waishi katika mazingira ambayo ni rafiki na hali zao.

 

TAHADHARI KWENYE SHUGHULI ZETU

Kama tulivyotangulia kuona hapo juu kuwa shughuli za kuwapatia watu rizikinazo zinaweza kuwa chanzo cha maradhi. Hivyo tahadhari maalumu zinatakiwa zitumike ili kuweza kujiepusha na madhara ambayo yangeweza kuthibitiwa. Kwa mfano uaweza kujikinga na baadhi ya adhari kwa kuvaa mavazi maalimu kama gkovs, gunboot makoti maalumu kulingana na kazi husika. Soma vizuri nembo za tahadhari unapofungua kifaa cha kufanyia kazi. Tahadhari zaidi zinategemeana na kazi yenyewe na sehemu husika.

 

TAHADHARI NA TABIA ZETU

Usafi w mwili ni katika tabia njema na ni rafikipia. Kuufanya mwili iwe na uwezo wa kujikinga. Usafi wa nguo ni njia tosha ya kupambana na maambukizo na maradhi mengineyo kama tulivyotoa mfano huko juu. Mtu anatakiwa kujenga tabia rafikia na afya kama kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi angalau mara tatu kwa wiki. Kutokuwa na abia ya kupenda vyakula vyenye chumvi nyingi hii huweza kumuepushha mtu na athari za kupata maradhi ya moyo kama presha na shambulio la moyo. Kupiga mswaki zaidi ya mara moja kwa siku na ukishindwa basi angalamu unapoamka na unapokwenda kulala. Tabia za kiafya zinaweza kujengwa kwenye vyakula, mazoezi, matendo na mazungumzo pia.

 

TAHADHARI JUU YA MARADHI YA KURITHI

Ni vigumu sana kujitahadhari kutopata maradhi haya kama kuwa albino. Ila inawezekana wazazi kulinda familia zao na maradhi ya kurithi ila pia ni ngumu. Kwani it itajika kupima kati ya wanandoa wawili kabla ya kupata watoto. Hapa ndio itaweza kugundulika maradhi haya ya kurithi kama yapo kwa wazazi na je upo uwezekano wa kuendelea kwa watoto. Kwa teknolojia iliyorahaisi kwa sasa ni kumlinda mtoto atakayezaliwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Ijapokuwa yapo matatizo mengine ya kurithi anaweza kukingwa mtoto akiwa tumboni asijedhurika. Tutaona zaidi matatizo haya kwenye kurasa zijazo.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-10-30     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1047


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Njia za kukabiliana na presha ya kupanda/hypertension
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kupanda Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO
Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu vitamini D na kazi zake mwilini
Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D. Soma Zaidi...

Namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi Soma Zaidi...

Kwanini mdomo unakuwa mchungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Soma Zaidi...

Mfuno wa damu na makundi manne ya damu na asili yake nani anayepasa kutoa damu?
Posti hii inakwenda kukujuza kuhusu makundi manne ya damu, asili yake, maana ya antijeni na antibody, pia utajifunza kuhusu mfumo wa Rh. Mwisho utajifunza watu wanaopasa kutoa damu. Soma Zaidi...

Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI
Somo hili linakwenda kukuletea mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia ugonjwa wa kipindupindu,
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kitaalamu huitwa vibrio cholera. Soma Zaidi...

Jinsi macho yanavyoweza kuzungumza kuhusu afya yako ya kimwili na kiakili
Soma Zaidi...

Faida za tumbo katika mwili wa binadamu
Posti hii inahusu zaidi faida za tumbo,tumbo ni sehemu ya mwili ambayo ushughilika na kutunza chakula, Soma Zaidi...

Ratiba ya chanjo ya kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hiii ni ratiba ambayo chanjo hii utolewa na ushauri mbalimbali utolewa ili kuweza kufanikisha kazi ya chanjo hii Soma Zaidi...