Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza ya mgonjwa mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo, ni Tiba ambayo utolewa kulingana na dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo kama ifuayavyo.
Tiba ya mgonjwa wa jeraha la kawaida kwenye ubongo
1.Kuangalia kama Kuna sehemu yoyote ambayo mgonjwa ameumia kwa sehemu ya nje inayoonekana Moja kwa Moja kwa macho kama Kuna damu ambayo inatoka,au kama Kuna kidonda kinachoonekana au kama Kuna kitu chochote ambacho kimejishikisha kwenye sehemu yoyote ya kichwa, kama vipo jaribu kuviondoa na kama Kuna kutokwa na damu jaribu kuzuia damu isitoke kwa kufanya hivyo unapunguza maumivu kwa mgonjwa.
2.Kumpatia mgonjwa mda wa kupumzika.
Mgonjwa anapaswa kupumzika Ili aweze kurudisha mfumo wa ubongo kwenye nafasi yake au kwenye kazi yake ya kawaida kwa mfano mgonjwa wa jeraha la kawaida kwenye ubongo utapika, uona kizunguzungu, uhisi kichefuchefu,kuona kwa shida au maruweruwe hayo yote utokea kwa sababu ya mshutuko kwenye ubongo kwa hiyo mgonjwa akipata mda wa kutosha wa kupumzika anarudisha kila kitu kwenye hali ya kawaida. Kwa hiyo wahudumu wanapaswa kujulishwa hilo Ili kumpa mgonjwa mda wa kupumzika.
3. Mgonjwa anapaswa kupewa dawa za kupunguza maumivu.
Kwa sababu ya maumivu kwenye kichwa na sehemu mbalimbali za mwili mgonjwa anapaswa kupewa dawa ya maumivu , lakini sio kila dawa za maumivu zinafaa kwa mtu Mwenye jeraha la kawaida kwenye ubongo kwa Sababu nyingine nyingine zinasababisha uvujaji wa damu kuongezeka kama vile Asprini na Ibuprofen mgonjwa hapaswi kuzitumia lla Panadol au paracetamol ni nzuri, kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kujua hilo.
4.Mwamshe mgonjwa mara kwa mara na mwoji maswali Ili kuona kama amerudisha fahamu.
Mgonjwa anapaswa kuamshwa na kuulizwa maswali kama vile uko wapi?, Unaumwa wapi?, Unataka nini?, Unaumia wapi? Kwa kufanya hivyo unaweza kuona tatizo la Mgonjwa liko wapi kwa sababu wakati mwingine mgonjwa aliyepoteza fahamu huwa tunamhudumia tunavyojisikia na pengine huwa tunaongeza maumivu bila kujua Ila kwa kumuuliza mgonjwa unaweza kupata njia ya kumlaza au kumgeuza. Kwa hiyo ni vizuri kumwuliza mgonjwa Ili upatiwe urahisi wa kumhudumia.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna mimba inavyotungwa mpaka mtoto kuingia kwenye mfuko wa uzazi, mimba kutungwa ni kitendo ambapo mbegu za kiume kuungana na yai la kike na kutengeneza zygote.
Soma Zaidi...Muulizaji anauliza he kula denda, ama kumbusu ama kufanya romance na muathirika was HIV na wewe uta ambukizwa?
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepaliwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi michubuko ambayo mara nyingi utokea kwa watoto wakati wa kuzaliwa,na mara nyingi uweza kupona baada ya masaa ishilini na manne au ndani ya masaa ishilini na manne.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na joto kubwa mwilini
Soma Zaidi...